Pata taarifa kuu

Senegal: Tume ya kitaifa yapendekeza kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Juni

Tume ya mazungumzo ya kitaifa nchini Senegal inapendekeza uchaguzi mkuu wa urais kufanyika tarehe 2 ya mwezi Juni mwaka huu hatua inayokuja baada ya tarehe ya awali kucheleweshwa.

Tume hiyo imeafikia mapendekezo hayo baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya siku mbili
Tume hiyo imeafikia mapendekezo hayo baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya siku mbili © Seyllou / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo hayo yanafuatia siku mbili za mazungumzo yaliyoandaliwa na Sall kwa lengo la kupunguza mvutano na kukubaliana juu ya njia ya kuondoka kwenye mzozo wa kisiasa wa takriban mwezi mzima.

Jaribio lake na la bunge lililoshindwa kuahirisha uchaguzi wa Februari 25 kwa miezi kumi limezusha machafuko na kauli za kutahadharisha juu ya kuporomoka  kwa demokrasia.

Mazungumzo hayo yaliofanyika katika mji mkuu wa Dakar yalisusiwa na wanasiasa wengi wa upinzani ambao baadhi yao wanataka uchaguzi ufanyike kabla ya muda wa kukaa madarakani rais  Macky Sall kumalizika tarehe 2 Aprili.

Taifa hilo lenye utulivu la Afrika Magharibi linapambana na mzozo wake mbaya zaidi wa kisiasa kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa baada ya Sall kuahirisha uchaguzi wa Februari 25 katika muda wa mwisho.

Baraza la Katiba lilibatilisha ucheleweshaji huo na siku ya Jumatatu Rais Sall alizindua mazungumzo ya siku mbili kuweka tarehe mpya, ambayo hata hivyo yaliyosusiwa na wahusika wakuu wa kisiasa na kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.