Pata taarifa kuu

Suala la usalama wa mashariki ya DRC limejadiliwa katika mkutano wa Luanda

Mazungumzo kuhusu hali inayojiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio yaliogubika mkutano wa Luanda, hapo jana kati ya Rais Félix Thisekedi wa DRC na mwenzake wa Angola Joao Lourenco, ambae pia mpatanishi katika mgogoro huu.

Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamezungumzia suala la usalama wa mashariki ya DRC.
Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamezungumzia suala la usalama wa mashariki ya DRC. © RDC
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unafuatia mkutano mdogo ulioandaliwa Februari 18 kando ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia lengo ikiwa ni kuwashawishi  marais wa Kongo na Rwanda kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zilizopo na kupunguza joto la uhasama unaoendelea.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Angola Tete Antonio, inasemekana rais  Félix  Tshisekedi amekubali  kimsingi kukutana na rais wa Rwanda, Paul Kagame, ikiwa sasa ni jukumu  la upatanisho kufanyia kazi mkutano huo.

Idara ya mawasiliano ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia inabainisha kuwa hakuna tarehe au eneo ambalo limepangwa kwa ajili ya mkutano huo iwapo utafanyika.

Paul Kagame wa Rwanda , João Lourenço wa Angola na Felix Thisekedi wa DRC katika mkutano wa awali
Paul Kagame wa Rwanda , João Lourenço wa Angola na Felix Thisekedi wa DRC katika mkutano wa awali AFP - JORGE NSIMBA

Hakuna rais hata mmoja aliezungumza baada ya mkutano huo wa ana kwa ana uliodumu kwa takriban saa tatu.

Kulingana na chanzo hicho hicho, wakati wa mkutano huu mdogo, mpatanishi Lourenço alionyesha nia yake ya kupata mkutano wa moja kwa moja kati ya mkuu wa nchi wa Kongo na mwenzake wa Rwanda.

Félix Tshisekedi alikuwa ametoa sharti la kufanyika kwa mkutano kama huo kwa kuondolewa mara moja kwa wanajeshi wa RDF katika ardhi ya Kongo, kusitishwa kwa mapigano na kuwekwa katika eneo moja kwa waqsi wa kundi la kigaidi la M23

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.