Pata taarifa kuu

Guinea: Vyama vya wafanyikazi vyasitisha mgomo wa kitaifa

Nairobi – Vyama vya wafanyikazi nchini Guinea vimetangazwa kusitishwa kwa mgomo wa kitaifa baada ya serikali kutimiza mojawapo ya sharti lao kuu la kumuachia huru kiongozi wa wanahabari katika muungano huo, Sekou Jamal Pendessa.

Sekou Jamal Pendessa- Kiongozi wa wanahabari katika muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini Guinea.
Sekou Jamal Pendessa- Kiongozi wa wanahabari katika muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini Guinea. REUTERS - Souleymane Camara
Matangazo ya kibiashara

Pendessa alikamatwa mwezi uliopita kwa makosa ya kulalamikia vikwazo vilivyokuwa vimetangazwa na utawala wa kijeshi ikiwemo kudhibitiwa kwa upatiakanaji wa intaneti pamoja na kufungiwa kwa baadhi ya stesheni za redio na televisheni.

Muungano wa vyama hivyo umesema utarejelea mazungumzo na serikali ya mpito kuhusiana na matakwa yao yaliosalia.

Waziri mkuu Mamadou Oury Bah, ambaye aliapishwa Jumanne ya wiki hii, alikuwa ametoa wito kwa vyama hivyo kusitisha mgomo huo akiahidi kushugulikia changamoto zao.

Vyama vya wafanyikazi nchini Guinea vinataka kupunguzwa kwa gharama ya bei za bidhaa pamoja na kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vilivyotangazwa na utawala wa kijeshi.

Guinea imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya mwezi Septemba mwaka wa 2021, uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika katika muda wa miezi 10 kurejesha utawala wa kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.