Pata taarifa kuu

Senegal: Wabunge wanajadili mswada wa kutoa msamaha kwa wafungwa wa kisiasa

Nairobi – Wabunge nchini Senegal wanajadili mswada wa kutoa msamaha kwa wale wote waliokamatwa na kushatakiwa kwa kuhusika na machafuko ya kisiasa kati ya Februari mwaka 2021 hadi Februari mwaka 2024.

Rais Macky Sall wa Senegal akiwa kwenye kikao cha mazungumzo ya kitaifa
Rais Macky Sall wa Senegal akiwa kwenye kikao cha mazungumzo ya kitaifa AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Mjadala huu unakuja, siku chache baada ya kupendekezwa na rais Macky Sall, kitendo ambacho wachambuzi wa siasa za Senegal wanasema ni mbinu ya kiongozi huyo kuwatuliza raia wa nchi hiyo baada ya kuarisha uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike mwezi uliopita.

Wanasiasa wa upinzani wamepinga mswada huu, wanaosema unalenga kuwakingia kifua, maafisa wa serikali hasa wale wa usalama waliohusika na mauaji ya waandamanaji na wengine waliojeruhiwa.

Iwapo mswada huo utapitishwa huenda, kukashuhudiwa kuachiwa huru kwa mwanasiasa maarufu Ousmane Sonko aliyefungwa  jela miaka mwaka uliopita na kusababisha maandamano makubwa nchini humo.

Senegal ambayo kwa miaka mingi, imeonekana kuwa mfano wa demokrasia barani Afrika, ipo kwenye njia panda ya kisiasa wakati huu uchaguzi mpya ukipendekezwa kufanyika tarehe 2 mwezi Juni, huku wanapinzani wakishikiza ufanyike kabla ya tarehe 2 mwezi Aprili, muhula wa rais Sall utakapofika tamati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.