Pata taarifa kuu

Kenya: Mpango wa kutuma polisi Haiti huenda ukakabiliwa na kizingiti tena

Nairobi – Mpango wa Kenya, kutuma polisi wake nchini Haiti, huenda ukawa matatani kwa mara nyingine, baada ya mwanasiasa mmoja nchini humo, kudai ataenda mahakamani kupinga makubaliano ya hivi karibuni kati ya serikali hizo mbili.

Kenya inalenga kuwatuma polisi elfu moja nchini Haiti
Kenya inalenga kuwatuma polisi elfu moja nchini Haiti REUTERS - THOMAS MUKOYA
Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa, Ekuru Aukot, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa, makubaliano kati ya Rais William Ruto na Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry ni batili na alishindwa kushughulikia pingamizi la jaji wa mahakama aliyezuia kutumwa kwa polisi hao.

Aukot amesemaa Henry, ambaye aliingia madarakani baada ya mauaji ya 2021 ya Rais Juvenal Moise, hana uhalali wa kisheria kuingia makubaliano hayo na kwamba sheria za Haiti zinazoongoza polisi hazifanani na zile za Kenya.

Waziri Mkuu wa Haiti,  Ariel Henry
Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry AP - Andrew Kasuku

Rais Ruto alisema katika hafla ya kutia saini siku ya Ijumaa kwamba, makubaliano na waziri mkuu Henry yataharakisha kuwasili kwa maafisa wa Kenya nchini Haiti, lakini serikali yake haijatoa ratiba au kuchapisha mpango huo.

Oktoba mwaka jana, Kenya ilikubali kuongoza Polisi wa kimataifa walioidhinishwa na Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo, ili kusaidia kukabiliana na magenge ya uhalifu yanayoihangaisha raia

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.