Pata taarifa kuu

Mkutano kati ya rais Kagame na Thsisekedi unaweza kufanyika hivi karibuni:Angola

Nairobi – Hali mashariki mwa DRC bado inazua mazungumzo makali ya kidiplomasia huku makabiliano yakiendelea kuwa makali kati ya M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, na wanajeshi wa Kongo. Siku ya Jumatatu, Rais wa Angola Joao Lourenço, mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika suala hili, alimpokea rais wa Rwanda mjini Luanda na kwa mujibu wa mamlaka ya Angola, mkutano kati ya Paul Kagame na Félix Thsisekedi unaweza kufanyika hivi karibuni.

Mazungumzo mapya kati ya viongozi hao wawili kwa hiyo yanaonekana kukaribia. Mkutano wao wa mwisho haukufaulu.
Mazungumzo mapya kati ya viongozi hao wawili kwa hiyo yanaonekana kukaribia. Mkutano wao wa mwisho haukufaulu. AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Ni Tété Antonio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, ambaye alitoa tangazo hilo siku ya Jumatatu kufuatia mkutano kati ya Rais wa Angola João Lourenço na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Waziri huyo aliwaambia wanahabari kwamba Rais Kagame atakubali kukutana na Rais Tshisekedi katika tarehe itakayopangwa na mpatanishi hivi karibuni.

Waziri wa Angola, hata hivyo, alichukua tahadhari kubainisha kwamba kila upande bado unapaswa "kufanya kazi katika kuwezesha hatua hii".

Ofisi ya Rais wa Rwanda haijathibitisha ahadi hiyo, ingawa ilithibitisha katika akaunti yake ya X kwamba "wakuu wa nchi wamekubaliana juu ya hatua muhimu za kuchukuliwa ili kukabiliana na sababu kuu za mzozo."

Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaotatiza usalama mashariki mwa DRC.
Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaotatiza usalama mashariki mwa DRC. © afp:Tchandrou Nitanga

Félix Tshisekedi alikubali kimsingi kukutana na mwenzake wa Rwanda, kulingana na taarifa ya Tété Antonio iliyochapishwa Februari 27 na Ikulu ya Kinshasa. Hata hivyo amekumbusha kwamba Rais Tshisekedi alikuwa ameweka masharti kadhaa kabla ya kufanyika kwa mkutano kama huo.

Mazungumzo mapya kati ya viongozi hao wawili kwa hiyo yanaonekana kukaribia. Mkutano wao wa mwisho haukufaulu.

Mnamo Februari 16 huko Addis Ababa, kando ya mkutano wa kilele wa AU, mkutano mdogo wa kilele kuhusu hali ya mashariki mwa DRC ulimalizika, kulingana na vyanzo kadhaa, na kubadilishana wachunguzi kati ya Félix Tshisekedi na Paul Kagame

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.