Pata taarifa kuu

Mambo ya kuzingatiwa na raia kuelekea uchaguzi mkuu wa urais nchini Senegal

Nairobi – Wakati huu nchi ya Senegal, ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 24 ya mwezi huu, kutafuta mrithi wa rais Macky Sall anayemaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa mihula miwili, masuala kadhaa yanaufanya uchaguzi huo kuwa muhimu zaidi kwa raia watakaoamua.

Uchaguzi mkuu wa urais kufanyika tarehe 24 ya mwezi huu.
Uchaguzi mkuu wa urais kufanyika tarehe 24 ya mwezi huu. © SEYLLOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Suala la kwanza ambalo wapiga kura watazingatia ni ajira, serikali ya sasa imekuwa ikituhumiwa kwa kushindwa kuunda nafasi za ajira, ambapo Vijana walio na umri wa chini ya miaka 25 ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya raia wa Senegal hawana ajira.

Vita vya Ukraine na athari zengine za ndani ya nchi kwa uchumi pia zimeripotiwa kuchangia mfumko wa bei, asilimia tatu ya raia milioni 17 wa Senegal wanaishi katika hali ya umaskini kwa mujibu wa data za benki kuu ya dunia.

Idadi kubwa ya raia wa Senegal pia wanamatumaini kuwa kiongozi anayekuja kati ya wagombea 19 wa urais atatatua suala la uhamiaji, wakati huu Raia wa Senegal na mataifa mengine ya Afrika Magharibi wamekuwa wakiripotiwa kuzama baharini wakijaribu kufika Ulaya.

Wapiga kura pia wanatarajia kuwa mrithi wa rais Macky Sall, ataimarisha uchumi wa Senegal kwa kutumia rasilimali zitakazotokana na kuanzishwa kwa uzalishaji wa mafuta na gesi baadae mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.