Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Niger yavunja makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani

Utawala wa kijeshi ulio madarakani nchini Niger ulishutumu siku ya Jumamosi makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani, yaliyoanza mwaka 2012, baada ya ziara ya siku tatu ya maafisa wakuu wa Marekani mjini Niamey.

Bendera za Marekani na Niger zinapepea katika kambi ya kijeshi huko Agadez, Niger, Aprili 16, 2018.
Bendera za Marekani na Niger zinapepea katika kambi ya kijeshi huko Agadez, Niger, Aprili 16, 2018. AP - Carley Petesch
Matangazo ya kibiashara

"Serikali ya Niger, kwa kuzingatia matakwa na maslahi ya raia wake, inaamua kwa wajibu wote kushutumu mara moja makubaliano yanayohusiana na hadhi ya wanajeshi wa Marekani na wafanyakazi wa kiraia wa Idara ya Ulinzi ya Marekani kwenye ardhi ya Niger,” alisema Amadou Abdramane, msemaji wa serikali ya Niger, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hii kwa vyombo vya habari, iliyosomwa Jumamosi jioni kwenye televisheni ya taifa, Bw. Abdramane anabainisha kuwa uwepo wa jeshi la Marekani ni "kinyume cha sheria" na "unakiuka sheria zote za kikatiba na kidemokrasia".

Kulingana na Niamey, mkataba huu unaoelezewa kuwa "sio wa haki" "uliwekwa kwa upande mmoja" na Marekani, kupitia "taarifa rahisi ya maneno", mnamo Julai 6, 2012.

Uamuzi huu unakuja muda mfupi baada ya kuondoka kwa ujumbe wa Marekani unaoongozwa na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika, Molly Phee.

Katika ziara hii ya siku tatu, Bi Phee hakuweza kukutana na mkuu wa utawala wa kijeshi Abdourahamane Tiani, kulingana na chanzo cha serikali ya Niger.

"Kuwasili kwa ujumbe wa Marekani hakuheshimu taratibu za kidiplomasia," alieleza Bw. Abdramane siku ya Jumamosi, na kuhakikisha kwamba serikali ya Marekani iliiarifu Niamey "upande mmoja" kuhusu tarehe yake ya kuwasili na muundo wa ujumbe wake.

Marekani ina wanajeshi zaidi ya 1,000 nchini Niger wanaohusika katika mapambano dhidi ya jihadi na kituo kikuu cha ndege zisizo na rubani huko Agadez (katikati)

Mara tu baada ya kuingia mamlakani kwa mapinduzi mnamo Julai 26, 2023, majenerali wa Niamey walishutumu makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Ufaransa.

Wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa waliondoka Niger mnamo Desemba 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.