Pata taarifa kuu

Senegal: Anta Babacar ni mwanamke peke anayewania katika uchaguzi wa Urais

Nairobi – Mwanamke pekee anayewania kiti cha urais nchini Senegal, Anta Babacar Ngom, anaweza asipewe nafasi kubwa sana ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma hili, lakini harakati zake zimesaidia kuongeza matumaini kwa wanawake walio wengi nchini humo.

Ni mwaka 2001  na 2012 Senegal ilipata mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi ya waziri mkuu.
Ni mwaka 2001  na 2012 Senegal ilipata mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi ya waziri mkuu. AFP - CARMEN ABD ALI
Matangazo ya kibiashara

Anta mwenye umri wa miaka 40, amekuwa sauti ya wanawake na vijana wanaokabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, ukosefu wa ajira na kupanda kwa gharama ya maisha, akiahidi kutengeneza mamilioni ya ajira ikiwa atachaguliwa.

Ni watu wachache wanampa nafasi mgombea huyu kuchaguliwa miongoni mwa vinara wanaopewa nafasi, lakini wanaharakati wanasema, ukweli kwamba amekuwa mwanamke wa Kwanza kuwania nafasi hiyo baada ya mwongo mmoja, inaoneshawanawake wanapiga hatua.

Anta mwenye umri wa miaka 40, amekuwa sauti ya wanawake na vijana wanaokabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi.
Anta mwenye umri wa miaka 40, amekuwa sauti ya wanawake na vijana wanaokabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi. © Tiemogo DIARRA/ RFI Mandenkan

Licha ya vikwazo anavyopitia kama mwanamke kutokana na tamaduni za nchi za Afrika Magharibi, Anta, amekuwa mfano wa wanasiasa wanawake ambao wamejipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii, kutokana na kuzungumzia masuala ambayo aghalabu hayajadiliwi na jamii ya Wasenegali.

Ni mwaka 2001  na 2012 Senegal ilipata mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi ya waziri mkuu, sheria ikitaka vyama kuzingatia usawa wa kijinsia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.