Pata taarifa kuu

DRC yapinga msaada mpya wa EU kwa Rwanda katika operesheni dhidi ya wanajihadi nchini Msumbiji

DRC inanyooshea kidole jukumu la Rwanda katika mgogoro wa M23 na kukemea sera ya Ulaya ya maridhiano kupindukia kuelekea Kigali.

Wanajeshi wa Rwanda.
Wanajeshi wa Rwanda. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Brussels, Laure Broulard

Brussels inaweza kutoa fedha zingine kusaidia operesheni za jeshi la Rwanda dhidi ya wanajihadi wa Ansar Al-Sunna huko Cabo Delgado (kaskazini mwa Msumbiji). Fedha zitakazotolewa ndani ya mfumo wa utaratibu wa Kituo cha Amani cha Ulaya zitajadiliwa kati ya wawakilishi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya katika wiki zijazo.

Lakini kwa upande wa Kinshasa, wanasema msaada huu mpya ungewakilisha "mstari mwekundu". Mwezi uliopita, kusainiwa kwa mkataba wa ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Rwanda kuhusu madini muhimu tayari kumeamsha hasira ya DRC, ambayo inashutumu jirani yake kwa kupora rasilimali zake. Kutolewa kwa ufadhili mpya kwa jeshi la Rwanda kwa hiyo kutakuwa "msaada kwa kikosi kinachotuhumiwa kuhusika katika mzozo wa Kivu Kaskazini" na "ishara nyingine ya ushirikiano kati ya Brussels na Kigali" ikinabaini chanzo kilicho karibu na ofisi ya rais wa Kongo.

Kwa upande wake, Brussels hivi karibuni ililaani uungaji mkono wa Kigali kwa M23 na kuhakikisha kupitia msemaji wake kwamba aina hii ya misaada haikusudii kuimarisha uwezo wa jumla wa jeshi la Rwanda, bali kuleta utulivu kaskazini mwa Msumbiji. Jeshi la Ulinzi la Rwanda linalinda eneo ambapo kampuni ya Ufarasa ya TotalEnergies inasubiri kuanza rasmi shughuli zake kwenye mradi mkubwa wa gesi asilia, uliositishwa mwaka 2021 kutokana na mashambulizi ya wanajihadi.

Bahasha ya kwanza ya euro milioni ishirini iliyokusudiwa kusafirisha wanajeshi wa Rwanda na ununuzi wa vifaa vya usafirishaji ilitolewa na Brussels mnamo mwaka 2022. Leo, Ufaransa na hata Ureno zinaunga mkono kanuni ya awamu ya pili wakati Ubelgiji na Uhispania zinasita zaidi kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa ofisi ya Ulaya ya shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch, Philippe Dam, anatoa wito kwa Umoja wa Ulaya kufuatilia kwa uwazi na kwa njia ya kuaminika matumizi ya ufadhili wake wa kwanza kabla ya kutoa fedha zingine. Shirika hilo lisilo la kiserikali linaamini kuwa uteuzi wa Jenerali Alex Kagame katika majira ya kiangazi mwaka jana kama mkuu wa kikosi cha Rwanda huko Cabo Delgado ulipaswa kuwa simulizi, kwani anashutumiwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuwa aliongoza operesheni mashariki mwa DRC mwaka 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.