Pata taarifa kuu

Wakuu wa SADC wanakutana nchini Zambia kujadili masuala ya kiusalama

Nairobi – Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Kusini mwa Afrika SADC wanakutana jijini Lusaka kwenye mkutano usiokuwa wa kawaida, kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Kaskazini mwa Msumbiji, pamoja na mambo mengine.

Rais FΓ©lix Tshisekedi aliwasili jijini Lusaka mapema leo kushiriki kwenye mkutano huo unaoongozwa na rais mwenyeji Hakaide Hichilema
Rais FΓ©lix Tshisekedi aliwasili jijini Lusaka mapema leo kushiriki kwenye mkutano huo unaoongozwa na rais mwenyeji Hakaide Hichilema Β© SADC
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja baada ya Jumuiya ya SADC kutuma wanajeshi wake mwezi Desemba mwaka uliopita nchini DRC, kupambana na makundi ya waasi hasa M 23 ambalo limeendelea kuwa tishio kwa usalama wa wakaazi wa Kivu Kaskazini.

Rais FΓ©lix Tshisekedi aliwasili jijini Lusaka mapema leo kushiriki kwenye mkutano huo unaoongozwa na rais mwenyeji Hakaide Hichilema.

Katika kikao hicho, viongozi wa nchi kutoka SADC wanaarifiwa kuhusu opresheni ya vikosi vya nchi hizo Mashariki mwa DRC na katika jimbo la Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji.

Mkutano huu unafanyika huku ripoti zikisema kuwa kuanzia siku ya Ijumaa, waasi wa M 23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda walipambana tena katika eneo la Bihambwe na viunga vyake, Wilayani Masisi.

Kuelekea mkutano huu, siku ya Alhamisi Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Rwanda na DRC walikutana jijini Luanda nchini Angola, kujadiliana kuhusu hali ya usalama, Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.