Pata taarifa kuu

Senegal: Bassirou Diomaye Faye kuapishwa siku ya Jumanne

Nairobi – Nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne baada ya kushinda uchaguzi wa urais wa Jumapili iliyopita, ambapo atakabiliwa na changamoto si haba za kutatua kutokana na matarajio makubwa.

Rais Mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye.
Rais Mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Muda tu baada ya kushinda uchaguzi, hotuba yake ya kwanza iligusia kupunguza gharama ya maisha, kupambana na ufisadi, kutafuta maridhiano ya kitaifa, ambapo siku ya Alhamisi alionesha ishara ya maridhiano kwa kukutana na rais anayeondoka Macky Sall.

Aidha Faye ameahidi kurejesha uhuru wa taifa hilo, kujadili upya mikataba ya mafuta na gesi, na kuboresha haki za uvuvi, lakini pia anaazimia kuondokana na matumizi ya faranga ya CFA, ambayo anaona ni urithi wa mkoloni wake Ufaransa.

Bassirou Diomaye Faye na ujumbe wake walikutana na rais anayeondoka madarakani, Macky Sall.
Bassirou Diomaye Faye na ujumbe wake walikutana na rais anayeondoka madarakani, Macky Sall. © AFP PHOTO / PRÉSIDENCE SÉNÉGALAISE

Hata hivyo wachambuzi wa uchumi, wanaona kuwa kibarua kikubwa kwa Faye ni kubuniwa kwa nafasi za ajira, hali ambayo imewafanya vijana wengi kuwa miongoni mwa wahamiaji wanaojaribu kuvuka na kuingia Ulaya.

Mtihani mwingine ni kurejesha imani ya wapiga kura, ambapo Faye anatakiwa kuwapa uthibitisho wa mapema wa nia yake kwa kupunguza haraka bei ya bidhaa kama vile mchele, mafuta na umeme.

Faye pia atalazimika kuamua iwapo atalivunja Bunge lililochaguliwa Septemba 2022, ambalo chama chake hakina wabunge wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.