Pata taarifa kuu

DRC: Askofu Mkuu wa Kishasa aishutumu serikali kwa kuwapa silaha FDLR

Kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kadinali Fridolin Ambongo ameionyoshea kidole cha lawama serikali ya DRC kwa kuwapa silaha si tu wanamgambo wa Wazalendo bali pia waasi wa Kihutu wa Rwanda wa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), wanaoendesha harakati zao katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kadinali Fridolin Ambongo Besungu, wakati wa misa ya Krismasi kwenye Kanisa Kuu la Notre-Dame du Congo mjini Kinshasa, Desemba 24, 2023.
Kadinali Fridolin Ambongo Besungu, wakati wa misa ya Krismasi kwenye Kanisa Kuu la Notre-Dame du Congo mjini Kinshasa, Desemba 24, 2023. © PATRICK MEINHARDT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, makundi kadhaa yanazuia kusonga mbele kwa waasi wa M23. Msaada huu wa serikali ya DRC kwa waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR tayari ulitajwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya (EU) na mabalozi wa nchi zingine, ingawa Kinshasa inakanusha. Hii ni zaidi ya hoja zote ambazo Rwanda inataja na hivyo kuonyesha uungaji wake mkono kwa waasi wa M23.

Askofu mkuu anathibitisha hili. Kwa kusambaza silaha zingine kwa maeneo mbalimbali, serikali inatumai kwamba “makundi haya yanaunga mkono jeshi dhidi ya kusonga mbele kwa M23.”

Kulingana na Fridolin Ambongo, "makundi haya yote yana silaha za kutosha" na "ni raia ndio hukutwa na matatizo". Askofu mkuu wa kanisa Katoliki nchini DRC anaona kuwa hali hi inaweza kusababisha "hatari ya ukosefu wa usalama wa jumla".

Askofu Mkuu wa Kinshasa analaani mkakati wa mamlaka iliyopo ambayo, badala ya "kuimarisha jeshi la taifa kwa askari waliochaguliwa na waliopewa mafunzo bora, inawapa silaha makundi yenye silaha" ambayo "huvamia raia, kutekeleza wizi na mauaji. "

Fridolin Ambongo anawashutumu wanamgambo wanaoshirikiana na wanajeshi wa serikali kujihusisha na biashara haramu ya madini ya DRC.

Kauli hii imeikasirisha Kinshasa. Thierry Monsenempwo, mmoja wa wasemaji wa muungano unaotawala, anasifu "ujasiri na kujitolea kwa wanaharakati wa Kongo wanaotetea amani huko Mashariki". Anamshutumu Askofu Mkuu wa Kinshasa kwa "kuzungumza lugha ya adui". Kulingana na Thierry Monsenempwo, "si haki kulinganisha wazalendo hawa wanaojitolea kutetea amani kwa makundi yenye silaha yanayoeneza ugaidi na vifo katika eneo hilo"

Kadinali Fridolin Ambongo alirejea Kinshasa siku ya Ijumaa, Aprili 19, baada ya siku tano akiwa ziarani huo Vatican. Aliponyimwa fursa ya kuingia kwenye chumba cha kusubiri cha watu mashuhuri katika uwanja wa ndege alipokuwa akisafiri nje ya nchi licha ya hadhi yake, alipita sehemu alipopitia kwa mara ya kwanza aliporejea nchini , kulingana na wasaidizi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.