Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Wawili wafariki na watatu kujeruhiwa kufuatia mabomu yaliyorushwa na M23 Kibirizi

Watu wawili walifariki na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mabomu yaliyorushwa Jumamosi Aprili 27 na waasi wa M23 huko Kibirizi, katika eneo la Rutshuru katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Wakaazi wa Bambo katika eneo la Rutshuru, kilomita 60 kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanatoroka makaazi yao wakati M23 ikishambulia mji huo Oktoba 26, 2023.
Wakaazi wa Bambo katika eneo la Rutshuru, kilomita 60 kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanatoroka makaazi yao wakati M23 ikishambulia mji huo Oktoba 26, 2023. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vya usalama vikinukuliwa na Redio OKAPI, kundi zima la mbuzi na nyumba nne pia ziliharibiwa na mabomu ya waasi hao.

Isaac Kibira, mashuhuri wa ufalme wa Bwito akinukuliwa na Redio OKAPI, alisikitishwa na hali hii na kuiomba serikali kufanya kila iwezalo kuukomboa mkoa huu:

“Ilikuwa mapema sana Jumamosi asubuhi ambapo Wazalendo walifanya uvamizi katika mji wa Kibirizi. Waliweza kudhibiti mji. Lakini kwa bahati mbaya, M23 ambayo iko katika nafasi ya kimkakati ilirusha mabomu na mabomu haya yakaharibu nyumba tatu. Raia wawili walifariki, na wengine watatu kujeruhiwa."

Halafu wakazi wa Kibirizi walijificha, wengine msituni na wengine walikaa majumbani kujikinga na mabomu haya.

Kwa hiyo, idadi kubwa ya waasi wa M23 walitokea Kishishe kuja kusaidia weneao ambao walikuwa Kibirizi.

Waasi hawa pia waliweka ngome huko Kabanda ili kukabiliana na wapiganaji wa Wazalendo.

"Tunaiomba Serikali kuwaondoa kwa nguvu waasi wa M23 katika eneo hili ili kuokoa maisha ya raia ambao wanajikuta katika mapigano ya wapiganaji," alihitimisha Isaac Kibira.

Kulingana na vyanzo vya usalama, kundi zima la mbuzi na nyumba nne pia ziliharibiwa na mabomu ya waasi hao.

Isaac Kibira, mashuhuri wa ufalme wa Bwito akinukuliwa na Redio OKAPI, alisikitishwa na hali hii na kuiomba serikali kufanya kila iwezalo kuukomboa mkoa huu:

“Ilikuwa mapema sana Jumamosi asubuhi ambapo Wazalendo walifanya uvamizi katika mji wa Kibirizi. Waliweza kudhibiti mji. Lakini kwa bahati mbaya, M23 ambayo iko katika nafasi ya kimkakati ilirusha mabomu na mabomu haya yakaharibu nyumba tatu. Raia wawili walifariki, na wengine watatu kujeruhiwa."

Halafu wakazi wa Kibirizi walijificha, wengine msituni na wengine walikaa majumbani kujikinga na mabomu haya.

Kwa hiyo, idadi kubwa ya waasi wa M23 walitokea Kishishe kuja kusaidia weneao ambao walikuwa Kibirizi.

Waasi hawa pia waliweka ngome huko Kabanda ili kukabiliana na wapiganaji wa Wazalendo.

"Tunaiomba Serikali kuwaondoa kwa nguvu waasi wa M23 katika eneo hili ili kuokoa maisha ya raia ambao wanajikuta katika mapigano ya wapiganaji," alihitimisha Isaac Kibira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.