Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Vyama mbalimbali vya siasa vyajiandaa vema katika Uchaguzi Mkuu wa Mei 29

Ni mwezi mmoja kamili leo kuelekea uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini, uliopangwa kufanyika tarehe 29 mwezi Mei.

Julius Malema kwenye jukwaa wakati wa mkutano wake huko Johannesburg Septemba 26, 2021.
Julius Malema kwenye jukwaa wakati wa mkutano wake huko Johannesburg Septemba 26, 2021. AFP - LUCA SOLA
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura Milioni 27 wanatarajiwa kupiga kura, kwenye uchaguzi huo ambao chama tawala ANC kinatarajiwa kupata ushindani mkali.

Kiongozi wa chama cha EFF Julius Malema, ni miongoni mwa wagombea urais na mwishoni mwa wiki iliyopita, aliendelea kufanya kampeni, Mashariki mwa jiji la Johannesburg.

"Tunaenda kupambana ili tuhakikishe kuwa tunapata ushindi tarehe 29 mwezi Mei, tutaondoa ufisadi Ikulu, huu ni wakati wenu wa kuweka historia na kuondoka kwenye shida na huu ndio wakati wetu wa kusimama imara" , amesema Julius Malema, mgombea urais kupitia chama cha upinzani cha  EFF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.