Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

DRC: Mapigano kati ya M23 na jeshi la Kongo yarindima mashariki mwa nchi

Nchini DRC, ghasia hazijapungua katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Baada ya mfululizo wa milipuko ya mabomu iliyogharimu maisha ya watu katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Goma, mapigano yameendelea kati ya vikosi vya serikali ya Kongo na M23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Mapigano yaliripotiwa wikendi hii katika eneo la Masisi ambayo yalisababisha tena watu kutoroka makaazi yao.

Wanajeshi wa jeshi la Kongo mashariki mwa DRC mnamo Juni 2022.
Wanajeshi wa jeshi la Kongo mashariki mwa DRC mnamo Juni 2022. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yaliripotiwa wikendi hii kusini mwa eneo la Masisi, karibu na mji wa Bitonga. Hali ya mashariki mwa DRC inatiwa wasiwasi mkubwa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika, SADC, ambayo kikosi chake kinatumwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumapili hii, Mei 5, SADC kwa upande mmoja ililaani milipuko ya mabomu kwenye kambi za watu waliohamishwa makazi yao, lakini pia ilitangaza kwamba itafanya operesheni na jeshi la Kongo "kuwazuia waasi wa M23, kudumisha amani kwa kuunda mazingira salama na njia wazi za usambazaji."

Idadi ya wanajeshi yaongezwa

Tangazo hili linakuja wakati kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Kongo, waasi wa M23 na wanajeshi wa Rwanda wanaendelea kutumwa kwa idadi kubwa katika eneo la vita. Jean-Pierre Bemba, wakati wa Baraza la Mawaziri siku ya Ijumaa Mei 3, alifahamisha serikali kwamba idadi ya wanajeshi na silaha mpya kutoka Rwanda zimesafirishwa, hasa kupitia mbuga ya wanyama ya Virunga.

Kama athari ya mapigano, wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa wanaendelea kukimbia kwa sehemu kuelekea kambi za watu waliokimbia makazi huko Goma ambako karibu watu milioni moja tayari wamekusanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.