Pata taarifa kuu

Senegal: Waziri Mkuu Ousmane Sonko ajiuzulu kwenye wadhifa wa meya wa Ziguinchor

Mawaziri waliokuwa na mamlaka ya kuchaguliwa walikuwa na hadi Jumapili Mei 5 kujiuzulu katika majukumu yao mengine. Tarehe ya makataa ya mwezi mmoja tangu kuteuliwa kwa serikali, ambayo ilitangazwa na Waziri Mkuu Ousmane Sonko ambaye mwenyewe amejiuzulu kutoka wadhifa wake kama meya wa Ziguinchor, kusini mwa nchi.

Ousmane Sonko, kiongozi wa chama cha PASTEF, mbele ya wanahabari katika shule ya msingi ya HLM huko Ziguinchor mnamo Julai 3, 2022.
Ousmane Sonko, kiongozi wa chama cha PASTEF, mbele ya wanahabari katika shule ya msingi ya HLM huko Ziguinchor mnamo Julai 3, 2022. Β© AFP - MUHAMADOU BITTAYE
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Dakar, ThΓ©a Ollivier

Waziri Mkuu Ousmane Sonko alitoa kauli ya mwisho kwa wajumbe wa serikali kuanzia jioni ya kuteuliwa kwao, Aprili 5: mawaziri wote ambao walikuwa na mamlaka ya kuchaguliwa walipaswa kujiuzulu katika majukumu yao mengine ndani ya mwezi mmoja, ili wajikite β€œhasa na majukumu yao ya kiserikali”. Kwa hivyo tarehe ya ambayo iliisha kitambo…

Tangu wakati huo, Ousmane Sonko mwenyewe ameonyesha mfano kwa kujiuzulu Jumamosi Mei 4 kutoka wadhifa wake kama meya wa mji wa Ziguinchor, jiji kuu la Casamance kusini mwa nchi, ambako amekuwa diwani tangu Januari 2022.

Waziri wa Nishati Birame Souleye Diop, ambaye alianzisha chama tawala cha PASTEF, pia alijiuzulu kama meya wa mji wa Thiès-Nord kulingana na Ousseynou Ly, msemaji wa ofisi ya rais.

Wa kwanza kuheshimu maagizo hayo ni Serigne Guèye Diop, Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye alijiuzulu kwenye wadhifa wake kama meya wa Sandiara, siku chache tu baada ya kuteuliwa kwake.

Maimouna Dièye, meya wa wilaya ya Patte d'oie huko Dakar na Cheikh Tidiane Dièye, naibu mwenyekiti wa baraza la Halmashauri ya Ziguinchor, bado hawajajiuzulu rasmi kutoka nyadhifa zao. "Wale ambao bado hawajafanya hivyo watafanya hivyo Jumatatu Mei 6," amesema Moustapha Sarré, msemaji wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.