Pata taarifa kuu

Senegal: Uchunguzi kuhusu ndege ya Boeing 737 kuwaka moto umeanzishwa

Mamlaka ya anga nchini Senegal, imeanzisha uchunguzi kuhusu tukio la ndege ya Boeing 737 kuwaka moto wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Dakar hapo jana, ambapo watu 11 wameripotiwa kujeruhiwa.

Ajali hiyo ndogo, ilisabababisha safari za ndege kukwama kwenye uwanja wa Kimataifa wa Blaise Diagne kwa muda.
Ajali hiyo ndogo, ilisabababisha safari za ndege kukwama kwenye uwanja wa Kimataifa wa Blaise Diagne kwa muda. © Zohra Bensemra / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo kutoka Shirika la ndege la Senegal inayomilikiwa na kampuni binafsi ya Transair, ilikuwa na abiria 78 waliokuwa wanaelekea jijini Bamako wakati, ilipokosa mwelekeo.

Ajali hiyo ndogo, ilisabababisha safari za ndege kukwama kwenye uwanja wa Kimataifa wa Blaise Diagne kwa muda, kabla ya kufunguliwa baadaye.

Mpaka sasa haijafahamika nini hasa kilichosababisha ndege hiyo kukosa mwelekeo, lakini mamlaka ya safari za ndege nchini Senegal zinasema, uchunguzi umeanza kubaini kilichofanyika.

Tukio hili limejiri wakati huu, Shirika la ndege nchini Senegal likiendelea kushtumiwa na abiria kwa miezi kadhaa sasa kwa kuchelewesha safari za ndani na nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.