Pata taarifa kuu

Sudan Kusini: Mapigano ya kikabila yazidi kuripotiwa katika kaunti ya Tambura

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, imetuma wanajeshi 300, kwenye Kaunti ya Tambura, eneo ambalo linashuhudia mapigano ya kikabila ili kutoa ulinzi kwa wakimbizi wa ndani zaidi ya Elfu tano.

Mapigano yakikabila yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Sudan Kusini.
Mapigano yakikabila yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Sudan Kusini. AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya wakimbizi hao ni wanawake, watoto na wazee, waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya mapigano hayo ya kikabila.

Papy Christian Tshienda ni mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa, kinachowashughulikia wakimbizi.

‘‘Tunafanya kila tunaloweza kusambaza vikosi vyetu hapa. Kutokana na ongezeko kubwa la wakimbizi wa ndani hapa Tambura na pia wanaoishi karibu na sisi tunawasaidia ipasavyo kwa kuwapa maji na mahitaji mengine na kuhakikisha kuwa tunashika doria kuimarisha usalama wao kambini wanaokoishi. ’’ Alisema Papy Christian Tshienda.

00:20

Papy Christian Tshienda ni mkuu wa kitengo cha UN kuhusu wakimbizi

Lucia Alfred ni mmoja wa wakimbizi, anaeleza changamoto wanazopitia.

‘‘Roho zetu kama mama tunahitaji kuishi na watoto wetu na tunataka wapate masomo kama watoto wengine ulimwenguni. Mwisho wa maisha Tambura umefika kwani hata kupata ndoo ya maji si rahisi. ’’ Alieleza Lucia Alfred ni mmoja wa wakimbizi.

00:17

Lucia Alfred ni mmoja wa wakimbizi

Kasisi Eduardo Kosala wa kanisa ya kikatoliki la Tambura, amekuwa msaada mkubwa kwa wakimbizi hao.

‘‘Siyo rahisi kukabiliana na hali iliyoko. Kuna silaha nyingi mikononi mwa watu. Watu wanaishi katika hali wasiwasi. Watu hawana chakula. Wasiwasi umetanda kote. Hali ya kukata tama imeenea kote. Watu wametoroka makwao. Wako hapa kwenye kanisa hili la Tambura.’’ Alieleza Kasisi Eduardo Kosala wa kanisa ya kikatoliki la Tambura.

00:21

Kasisi Eduardo Kosala wa kanisa ya kikatoliki la Tambura

Siku chache zilizopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress kwenye ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuendelea kwa mapigano mengine ya kikabila kwenye jimbo la Abyei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.