Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Wanane wauawa katika shambulizi la ADF kwenye kituo cha afya mashariki mwa DRC

Takriban raia wanane, wakiwemo wagonjwa waliokuwa kwenye vitanda vyao vya hospitali, waliuawa Jumatano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa shambulio dhidi ya kituo cha afya na waasi wa ADF, kundi lenye mafungamano na kundi la Islamic State, duru za ndani zimesema hivi punde sku ya Alhamisi usiku.

Wanajeshi wa FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) wakati wa operesheni dhidi ya waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) huko Opira, Kivu Kaskazini, Januari 25, 2018.
Wanajeshi wa FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) wakati wa operesheni dhidi ya waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) huko Opira, Kivu Kaskazini, Januari 25, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Adui" alikuja kutoka mkoa wa Ituri na kufanya shambulia mapema jioni huko Mantumbi, katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini, Omar Kalisia, kiongozi wa mashirika ya kiraia katika eneo la Beni, amewaambia waandishi wa habari.

"Kwa sasa, tuna idadi ya vifo vya watu wanane, ikiwa ni pamoja na wagonjwa na mhasibu wa kituo cha afya," amesema, na kuongeza kuwa muuguzi mmoja hajulikani aliko. Nyumba pia ilichomwa moto.

Pia akihusisha shambulio hili na ADF, Léon Siviwe, mkuu wa eneo moja huko Beni, kwa upande wake amesema watu kumi ndio waliuawa katika shambulio hilo, akiwemo muuguzi mmoja kulingana na kiongozi huyo. "Hatukuelewa chochote kwa sababu ngome ya UPDF (jeshi la Uganda) iko karibu wa mita chache, na eneo la tukio" ameliambia shirika la habari la AFP.

Tangu mwisho wa mwaka 2021, majeshi ya Kongo na Uganda yamekuwa yakifanya operesheni ya pamoja dhidi ya ADF ("Allied Democratic Forces") katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Kundi la waasi wa ADF, ambalo wengi wa wapiganaji wake ni Waislamu, limeanzishwa tangu katikati ya miaka ya 1990 mashariki mwa DRC, ambapo wameua maelfu ya raia na katika wiki za hivi karibuni kuongeza mashambulizi dhidi ya vijiji, wasafiri na vituo vya afya, mara nyingi kuporwa.

Mnamo mwaka 2019 walitangaza kujiunga na ISIS, ambayo inawatambulisha kama "jimbo lake la Afrika ya Kati" (ISCAP), na pia wanashutumiwa kwa mashambulizi ya hivi karibuni katika ardhi ya Uganda.

Watu watatu waliuawa na washukiwa wa ADF siku ya Jumanne huko Ituri, ambapo raia wengine wawili waliuawa siku ya Alhamisi "katika shambulio la kuvizia" lililotekelezwa na waasi kwenye barabara ya kitaifa ya 4 katika eneo la Irumu, kulingana na afisa wa shirika la kutetea haki za binadamu katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.