Pata taarifa kuu
URENO

Chama cha upinzani nchini Ureno cha Socialist Democratic chashinda uchaguzi mkuu

Chama kikuu cha upinzani nchini Ureno cha Socialist Democtratic kinachoongozwa na Pedro Passos Coelho kimeshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo na kukibwaga chama kilichokuwa kikitawala cha Socialist cha waziri mkuu Jose Socrates.

Kiongozi wa chama cha Socialist Democratic, Pedro Passos Coelho
Kiongozi wa chama cha Socialist Democratic, Pedro Passos Coelho Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa na upinzani mkali umeshuhudiwa chama cha Socialist Democratic (PSD) cha bwana Pedro Passos Coelho kikishinda uchaguzi huo kwa kupata ushindi wa asilimia 38.6 dhidi ya chama cha Socialist cha waziri mkuu Jose Socrates kilichopata ushindi wa asilimia 28 wakati chama kingine cha Conservative CDS-PP kikipata asilimia 11.7.

Tayari bwana Jose Socrates wa chama kilichokuwa kinatawala nchini humo amekubali kushindwa katika uchaguzi huo na kutoa pongezi kwa chama cha upinzani ambacho sasa ni lazima kitafute ushirika na chama cha Conservative ili kuweza kuunda serikali ya umoja.

Kushindwa kwa chama tawala nchini humo kumeelezewa kuwa ni kutokana na chama hicho kushindwa kutekeleza vema sera za umoja wa ulaya ikiwa ni pamoja na viongozi wake kushindwa kukabiliana na hali ngumu ya maisha kwa wananchi wake na kushindwa kukuza hara uchumi wa taifa hilo.

Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini humo wanasema kuwa pia nchi hiyo kuonekana mzigo katika umoja wa ulaya ni jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kusababisha chama hicho kushindwa uchaguzi huo ambapo awali waziri mkuu Socrates alitangaza kuomba mkopo toka umoja wa ulaya wa zaidi ya dola milioni 80 kuisaidia nchi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo kiongozi wa chama cha upinzani kilichoshinda uchaguzi huo Pedro Passos Coelho ameapa kuhakikisha chama chake kinatekeleza maazimio ambayo yalikuwa yamependekezwa na umoja wa ulaya ili nchi hiyo iweze kuaptiwa mkopo.

Katika hotuba yake hiyo pia amewahaidi wananchi wake pamoja na nchi wanachama zilizoko katika umoja wa ulaya kuwa serikali yake haitataka kuwa mzigo kwa mataifa hayo kwa kuwa inakopa fedha hizo bali atahakikisha mkopo huo unatumika kufufua uchumi wa taifa hilo na kuleta mabadiliko.

Moja ya msharti ambayo yalikuwa yametolewa na umoja wa ulaya kwa nchi hiyo ili iweze kupatiwa mkopo huo ni pamoja na kupunguza kodi, kusitisha malipo ya pensheni, kupunguza mishahara na kukabilina na ukosefu wa ajira pamoja na umri wa kustaafu kazi.

Kufuatia chama chake kushindwa katika uchaguzi huo, bwana Socrates ametangaza kuachia madaraka ya uenyekiti wa chama hicho kama njia moja wapo ya kuonyesha uwajibikaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.