Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA

Israel yashambulia anga la Palestina na kuua wapiganaji 12

Wapiganaji kumi na wawili ambao ni raia wa palestina wameuawa huku watu ishirini wakijeruhiwa kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya anga katika ukanda wa gaza,madaktari kutoka Palestina wamethibitisha.

Moja ya athari za  mashambulizi ya anga yaliyojiri katika ukanda wa Gaza
Moja ya athari za mashambulizi ya anga yaliyojiri katika ukanda wa Gaza REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kwa vyanzo vya kijeshi vya israel inafafanua kuwa mashambulizi ya anga yalijiri mara 13 yakielekezwa eneo lengwa ikiwa ni pamoja na kwa kiongozi wa majeshi.

Uvamizi huo wa israel unakuja kufuatia mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na palestina kusini mwa israeli tangu ijumaa asubuhi na kujeruhi watu wanne.

Mapema jumamosi majeshi ya Israel yamearifu kuwa Mashambulizi hayo ya anga yalilenga viwanda viwili vya uzalishaji wa silaha kaskazini mwa gaza, katikati mwa ukanda huo na eneo lenye shughuli za kigaidi kusini mwa ukanda wa gaza.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.