Pata taarifa kuu
BAHRAIN

Mahakama ya Rufaa Nchini Bahrain yataka kesi inayowakabili Wanaharakati 21 isikilizwe upya

Mahakama ya Rufaa Nchini Bahrain imetoa amri ya kusikilizwa na kutolewa upya kwa hukumu katika kesi inayowakabili Wanaharakati ishirini na moja akiwemo Abdulhadi Al Khawaja ambaye anaendelea na mgomo wake wa kula wakati akitumikia kifungo kwa kosa la kuhusika kwenye maandamano ya kushinikiza mabadiliko ya utawala. Shirika la Habari la Umma Nchini Bahrain BNA limetoa taarifa hiyo na kusema Mahakama ya Rufaa imeagiza mara moja ushahidi uchukuliwe upya kutoka kwa Mwendesha Mashtaka na hata mashahidi warejee tena Mahakamani ili kusikilizwa kwa kesi hiyo na hatimaye hukumu ndiyo itolewe.

Waandamanaji nchini Bahrain ambao wamekuwa wakiendelea kupingana na utawala kwa kufanya maandamano kila uchao
Waandamanaji nchini Bahrain ambao wamekuwa wakiendelea kupingana na utawala kwa kufanya maandamano kila uchao REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na Wanaharakati hao ambao walishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha mabadiliko ya kiutawala nchini Bahrain yanafanyika kipindi ambacho nchi za Kiarabu zilikuwa zinapita kwenye wimbi la mabadiliko miezi kumi na minne iliyopita.

Mahakama ya Rufaa kwenye hukumu hiyo haijasema iwapo wanaharakati hao ambao kwa sasa wanashikiliwa wataachiwa kipindi ambacho kesi yao inastahili kuszilizwa upya kabla ya kutolewa hukumu au watendelea kushikiliwa kwa muda wote ambapo kesi hiyo itakuwa inasikilizwa upya.

Mahakama ya Rufaa nchini Bahrain ilikubali rufaa ambayo ilikatwa na Wanaharakati wa Kutetea Haki za Binadamu wakipinga hukumu ambayo ilitolewa na Mahakama ya Kijeshi dhidi ya wanaharakati ishrini na moja wakiwemo Khawaja na Ibrahim Sharif.

Kesi hiyo inarudi tena Mahakama kwa ajili ya kusikilizwa lakini tarehe ya kuanza upywa kwa mashtaka hayo yaijawekwa bayana lakini Mwanasheria wa Wanaharakati hao amesema anaimani katika kipindi cha majuma machache kesi hiyo itarejea upya Mahakamani.

Hukumu ya awali iliwapa kifungo cha maisha Khawaja na Wanaharakati wengine saba kwa kosa la kushiriki kwenye maandamano ya kutaka kuuangusha utawala wa Kifalme wa Bahrain mapema mwaka jana.

Watu wanaokadiria kufikia hamsini walipoteza maisha kwenye machafuko hayo yaliyotokea mwezi February mwaka elfu mbili na kumi na moja huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kwenye maandamano yaliyokuwa yanakutana na upinzani wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.