Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya wataka kura ya maoni Zimbabwe kuondoa vikwazo

Umoja wa Ulaya EU umesema kwamba utaiondolea vikwazo nchi ya Zimbabwe iwapo nchi hiyo itaandaa kura ya maoni kuhusu katiba ili kuitisha uchaguzi wa rais uliohuru wa haki na kidemokrasia.

Reuters/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa Ulaya wamekutana jana jijini Brusels kujadili jambo hilo.

Mbali na kuiondolea vikwazo Zimbabwe, Umoja wa Ulaya umesema utaanzisha ushirikiana wa moja kwa moja na nchi hiyo katika sekta ya maendeleo.

Chama cha Rais Robert Gabriel Mugabe kimesema vikwazo hivyo havitakiwi kuwepo, na vinatakiwa kuondolewa bila masharti yoyote.

Mugabe kwa kipindi kirefu amekua akitofautiana na msimamo wa nchi za magharibi na Ulaya na hivyo nchi yake kuwekewa vikwazo ambavyo vimekua ni mwiba kwa maisha ya wananchi wa kawaida.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.