Pata taarifa kuu
DRCONGO-UN

Walinda amani wa umoja wa mataifa washindwa kuwadhibiti waasi huko DRC.

Helikopta za mashambulizi za walinda amani wa umoja wa mataifa jana Jumamosi zilishindwa kuwazuia waasi kuteka mji mwingine huko Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, wakati baraza la usalama likifanya kikao kingine cha dharura kuhusu mgogoro huo 

Walinda amani wa umoja wa mataifa
Walinda amani wa umoja wa mataifa cbc.ca
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo serikali ya Kinshasa imetoa shutuma mpya dhidi ya nchi ya Rwanda na kusema kuwa inafadhili vikosi vya uasi mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa kikosi cha walinda amani wa umoja wa mataifa amesema kuwa waasi wa kundi la m23 walifanikiwa kuuteka mji wa Kibumba unaopatikana umbali wa kilomita 25 Kaskazini mwa Goma.

Waasi wa kundi la M23 wametangaza kuushika mji wa Kibumba kilomita ishirini Kaskazini mwa Goma jimboni Kivu ya Kaskazini ambapo baadhi ya raia wahamiaji tayari wameanza kubomoa makazi yao na kukimbilia mjini Goma.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.