Pata taarifa kuu
DRC-UGANDA

Waasi wa M23 watangaza utayari wao wa kusaini makubaliano na Serikali ya DRC kwenye mazungumzo huko Uganda

Waasi wa Kundi la M23 ambao wanapambana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC katika eneo la Mashariki wametangaza utayari wao wa kusaini mkataba wa makubaliano na serikali kama Kinshasa itakuwa tayari kwa hilo.

Kiongozi wa Ujumbe wa Kundi la Waasi la M23 kwenye mazungumzo na Serikali huko Kampala François Rucogoza
Kiongozi wa Ujumbe wa Kundi la Waasi la M23 kwenye mazungumzo na Serikali huko Kampala François Rucogoza REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Kundi la M23 limetangaza hatua hiyo kipindi hiki ambacho ujumbe wake upo nchini Uganda kwa mazungumzo na Serikali ya Kinshasa licha ya hadi sasa pande hizo mbili kushindwa kuanza mazungumzo hadi leo.

Msemaji wa Kisiasa wa Kundi la M23 Bertrand Bisimwa amesema wao wametumwa na wananchi wa DRC ambao wanahitaji amani na wamechoshwa na machafuko na ndiyo maana wameonesha utayari wa kusaini makubaliano na serikali.

Bisimwa ameweka bayana safari yao na Viongozi wa serikali ya Kinshasa huko Kampala si ya kwenda kukaa kwenye mahoteli bali kuangalia ni kwa namna gani watamaliza machafuko yanayoendelea kuwa kero huko Mashariki mwa DRC.

Msemaji huyo wa Kisiasa wa M23 pia ameendelea kukanusha vikali madai ya wao kupata ufadhili kutokwa kwa serikali ya Kampala ambao unawasaidia kuendeleza mapambano dhidi ya serikali ya Kinshasa.

Bisimwa amesema hayo ni maneno ambayo yanasambazwa na serikali kwa lengo la kchafua taswira yao mbele ya Jumuiya ya Kimataifa na imekuwa chanzo cha wao kuwekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika hatua nyingine mazungumzo baina ya Viongozi wa Serikali ya Kinshasa na Kundi la M23 yanatarajiwa kuanza hii leo baada ya malumbano yaliyodumu kwa zaidi ya majuma mawili baina ya pande hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Raymond Tshibanda amesema mazungumzo hayo yataanza baada ya kushughulikiwa kwa baadhi ya mambo yanayotajwa kama chanzo cha kushindwa kufikiwa muafaka baina ya pande hizo mbili.

Mpatanishi wa mgogoro wa DRC ni Waziri wa Ulinzi Crispus Kiyonga amesema viongozi wataendelea na mazungumzo hayo licha ya kuanza kulaumiwa kuwa chanzo cha kusababisha mazungumzo hayo yanakwama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.