Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Wananchi wa Zimbabwe wakaribia kupata Katiba Mpya baada ya Bunge nchini humo kupitisha muswada huo

Bunge nchini Zimbabwe limeidhinisha muswada wa katiba ambao ni sehemu ya upatikana wa katiba mpya nchini humo iliyopigiwa kura ya ndiyo na asilimia tisini ya wananchi wa Taifa hilo mapema mwezi Machi.

Wabunge hawa wa Zimbabwe ni miongoni mwa waliopitisha muswada wa katiba mpya
Wabunge hawa wa Zimbabwe ni miongoni mwa waliopitisha muswada wa katiba mpya
Matangazo ya kibiashara

Wabunge 156 kati ya 210 walipigakura ya kupitishwa kwa mswada huo ikiwa ni zaidi ya theluthi mbili kama ambavyo sehrai inavyotaka na hivyo sasa jukumu litaelekezwa kwa Baraza la Seneti.

Spika wa Bunge Lovemore Moyo amesema muswada huo umepitishwa na Bunge lake na sasa kazi itaelekezwa kwa Baraza la Seneti ambalo likipitisha ndipo Rais Robert Mugabe ataisaini na kuwa sheria.

Hatua ya Rais Mugabe kuweka saini baada ya kupitishwa na Baraza la Seneti itakuwa imefungua ukurasa mpya kwa Zimbabwe kupata katiba mpya na kumalizika kwa muda wa katiba ya zamani iliyotumika tangu mwaka 1980.

Spika amesema wabunge wote waliokuwemo walipiga kura ya kupitisha muswada huo ukiondoa wale waliokosekana na waliokimbia mchakato huo wa upigaji wa kura ya kupitisha muswada wa katiba.

Iwapo Baraza la Seneti litapitisha muswada huo na Rais Mugabe kuasini kuwa sheria itaashiria wananchi wa Zimbabwe wataingia kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Julai wakitumia katiba hiyo mpya.

Katiba hiyo mpya imekuwa ikililiwa kwa muda mrefu na wapinzani ambao wamekuwa wakilalama chaguzi zimekuwa zikiendeshwa kwa upendeleo wa kukisaidia Chama Tawala cha ZANU-PF.

Kuanza kutumika kwa katiba hiyo mpya inaweza ikawa msumari wa moto kwa Chama Cha ZANU-PF ambayo sasa itakuwa inakutana na vipingamizi vinavyoonekana suluhu ya uongozi na Chama cha MDC.

Katiba mpya inapunguza madaraka ya rais na kuondoa kinga ya kushtakiwa kwa kiongozi huyo pindi anapoondoka madarakani, mahakama itapewa nguvu zaidi, inataka kuundwa kwa Tume ya maridhiano, kupunguzwa kwa muda wa rais kuongoza na kufutwa kwa nafasi ya Waziri Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.