Pata taarifa kuu
UMOJA WA ULAYA

Idadi ya watu wasio na ajira barani Ulaya yazidi kuongezeka, sasa ni tishio kwa ukuaji wa uchumi wa ukanda huo

Takwimu mpya za ajira barani Ulaya zimeonesha kuna uongezeko kubwa la watu wasio na ajira na kuendelea kuwa tishio kwa ukuaji wa uchumi wa mataifa ya nchi wanachama.

Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana limekuwa tishio la ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya
Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana limekuwa tishio la ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya Reuters
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizo zinaonesha kuwa ongezeko la watu wasio na ajira limekuwa likipanda kila mwezi huku kwa mwezi wa tatu ikirekodi ukosefu wa ajira kwa asilimia 12.1 kabla ya kupanda kwa mwezi wa April hadi kufika asilimia 12.2.

Ripoti mpya inaonesha kuwa mpaka kufikia mwezi May kumekuwa na ongezeko la watu wasio na ajira wanaofikia elfu 95 katika nchi kumi na saba wanachama wa Umoja huo na kufanya idadi hiyo kufikia watu milioni 19.38 wasio na ajira kwenye ukanda wa Euro.

Nchi za Ugiriki na Uhispania zenyewe zimeendelea kurekodi idadi kubwa ya watu wasio na ajira kwa kiwango cha asilimia 25 huku nchi ambayo imefanikiwa kutengeneza ajira na kuwa na idadi ndogo ya watu wasio na ajira ni Austria ambayo tatizo la ukosefu wa ajira ni asilimia 4.9.

Kwa mujibu wa taarifa ya taasisi ya Umoja wa Ulaya ya Eurostat inasema kuwa nchi ya Ujerumani imerekodi tatizo hilo kwa asilimia 5.4 huku Luxembourg ikirekodi watu wasio na ajira kwa asilimia 5.6.

Kiwango kikubwa zaidi kwa nchi wanachama kuwa na watu wengi wasio na ajira ni nchi ya Ugiriki yenye asilimia 27.0 mpaka kufikia mwezi February mwaka huu, Uhispania ikafikia asilimia 26.8 na Ureno asilimia 17.8

Takwimu hizo zinatolewa wakati huu ambapo viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wamekubaliana kuhakikisha wanafufua soko la ajira kwa cnhi wanachama ili kukabiliana na ongezeko kubwa la watu wasio na ajira ili kunusuru uchumi wake.

Viongozi hao pia wamekubaliana na wazo la kuwa na kiongozi wa kudumu wa Umoja wa Ulaya kuliko ilivyo hivi sasa ambapo huchaguliwa kulingana na kipindi maalumu na uteuzi wake hutegemea kura za nchi wanachama.

Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana limeendelea kuwa kikwazo cha ukuaji wa uchumi wa mataifa ya ukanda wa Ulaya hasa kwa mwezi April mwaka huu kwa vijana walio na umri wa kati ya miaka 25 wakitajwa kuwa waathirika wakubwa wa kukosa ajira ambao idadi yao inafikia milioni 3.6 sawa na asilimia 24.4.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.