Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Mahakama ya katiba nchini Zimbabwe yamwagiza rais Mugabe kuandaa uchaguzi mkuu kabla ya tarehe 31 July

Mahakama kuu ya katiba nchini Zimbabwe imemuagiza rais Robert Mugabe kupanga tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na ule wa Serikali za mitaa, kabla ya tarehe 31 ya mwezi July.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akitia saini katiba mpya huku waziri mkuu Morgan Tsvangirai akitazama
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akitia saini katiba mpya huku waziri mkuu Morgan Tsvangirai akitazama Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahabari mjini Harare Zimbabwe jaji mkuu Godfrey Chidyausiku amesema kuwa mahakama kuu imemuagiza rais Robert Mugabe kuandaa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kabla ya tarehe 31 ya mwezi July mwaka huu.

Uamuzi huo wa mahakama unakuja wakati huu ambapo toka rais Mugabe amesaini na kuwa sheria kuanza kutumika kwa katiba mpya, bado serikali ya umoja wa kitaifa haijatangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu licha ya kuwa ilitangazwa kuwa ni mwezi July.

Kufanyika kwa uchaguzi huo kutamaliza utawala wa Serikali ya muungano kati ya chama cha ZANU-PF na kiel cha Upinzani cha MDC kinachoongozwa na waziri mkuu Morgan Tsvangirai ambapo waliunda Serikali hiyo mwaka 2009.

Wananchi wa Zimbabwe wanatarajiwa kushiriki zoezi la uchaguzi mkuu wa nchi hiyo chini ya katiba mpya iliyotiwa saini na rais Mugabe juma moja lililopita na kuwa sheria.

Upinzani na wanaharakati nchini Zimbabwe umekuwa kwa muda mrefu ukipigia kelele kufanyika mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo ikiwemo kuwa muhula maalumu kwa rais kukaa madarakani.

Rais Mugabe anatarajiwa kusimama tena kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi huo ambapo upinzani chini ya chama cha ZANU-PF unatarajiwa kumsimamisha waziri mkuu Morgan Tsvangirai.

"The first respondent (Mugabe) be hereby ordered and directed to proclaim as soon as possible a date for the holding of presidential elections, general elections and elections of members of governing bodies of local authorities... which elections should take place no later than the 31st of July 2013," Chief Justice Godfrey Chidyausiku said.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.