Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Wafuasi wa raisi Sata wawashambulia wanaharakati Zambia

Wafuasi wanaounga mkono chama tawala nchini Zambia wamewashambulia kwa kipigo wanaharakati ambao walihamishia kanisani maandamano yao yaliyolenga kupinga bei kubwa ya vyakula baada ya mpango wao wa maandamano kupigwa marufuku.

Raisi wa Zambia Michael Sata
Raisi wa Zambia Michael Sata www.swradioafrica.com
Matangazo ya kibiashara

Takribani wanaharakati 60 wa kijamii wakiwemo wanasiasa wa upinzani walikusanyika katika kanisa moja mjini Lusaka wakiimba ndipo takribani wafuasi mia moja wa raisi wa Zambia Michael Sata walifika na kuanza mashambulizi dhidi ya wanaharakati hao.

Askofu John Mambo, ambaye amekuwa akitoa changamoto kali kwa raisi Sata alijeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa shoka na kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Ombi la wanaharakati hao kufanya maandamano lilipigwa marufuku na jeshi la polisi nchini humo kutokana na sababu za kiusalama na kulazimika kuhamishia maandamano kanisani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.