Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe asisitiza uchaguzi kufanyika mwishoni mwa Julai licha ya Wapinzani kutaka usogezwe mbele

Serikali ya Zimbabwe imesisitiza uchaguzi mkuu utafanyika mwishomi mwa mwezi Julai kama ambavyo umepngwa licha ya Upinzani kudai uchaguzi huo usogezwe mbele hadi pale ambapo mabadiliko muhimu yatakuwa yamefanyika.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye ametangaza kugombea tena Urais kwenye uchaguzi utakaofanyika tarehe 31 Julai
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye ametangaza kugombea tena Urais kwenye uchaguzi utakaofanyika tarehe 31 Julai Reuters/Philimon Bulwayo
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amesema baada ya kupatikana kwa katiba mpya huu sasa ni wakati muafaka kwa nchi hiyo kuandaa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 ya mwezi Julai.

Tamko la Rais wa Mugabe limekosolewa vikali na Waziri Mkuu ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Morgan Tsvangirai huku akisema uchaguzi huo haufai kufanyika kwa sasa kwa kuwa bado kunahitajika mabadiliko zaidi muhimu.

Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe ndiyo ilitangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mwishoni mwa juma tamko lililopokelewa kwa mikono miwili na Rais Mugabe aliyetangaza kuwania wadhifa wake kwa mara nyingine.

Mugabe alijitokeza kwenye mahojiano yaliyofanyika kwenye radio na kusema hatimaye wakati wa kufanyika uchaguzi umewadia na hivyo kutaka kila mtu kuheshimu sheria ili uchaguzi huo ufanyike kwa mafanikio makubwa.

Msemaji wa Waziri Mkuu Tsvangirai, Luke Tamborinyoka amesema Mahakama ya Katiba imepiga hatua zaidi tofauti na ilivyopaswa kufanya katika kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa haki na usawa.

Tamborinyoka kupitia taarifa yake amesema Mahakama ya katiba haina mamlaka ya kupanga tarehe ya uchaguzi kwa kuwa hilo ni jukumu la Tume Huru ya Uchaguzi ndiyo maana wanashangaa ni kwa nini wamenyang'anywa nafasi hiyo.

Rais Mugabe ametoa wito kwa Vyombo vya Usalama, Vyombo vya Habari na Tume ya Uchaguzi kuhakikisha wanasimama kidete ili nchi ya Zimbabwe ifanye uchaguzi uliohuru na wa haki utakaosaidia kupatikana kwa Viongozi wajao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.