Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe ZEC yaanza kutangaza matokeo

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe ZEC hatimaye imeanza kutangaza matokeo ya viti vya ubunge kabla ya kutangaza matokeo ya urais ambayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi wa Zimbabwe na dunia kwa ujumla.

Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai ambaye pia ni kiongozi wa upinzani amejitokeza kwa wanahabari na kusema uchaguzi haukuwa huru na haki.
Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai ambaye pia ni kiongozi wa upinzani amejitokeza kwa wanahabari na kusema uchaguzi haukuwa huru na haki. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Makamu mwenyekiti wa tume hiyo, Joyce Kazembe amesema matokeo hayo yataendelea kutangazwa kadiri watakavyokuwa wakiyapokea na kwamba yakimalizika matokeo ya majimbo yote ndipo wataanza kutangaza matokeo ya raisi.

Wakati matokeo haya yakitangazwa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC-T kupitia rais wake Morgan Tsvangirai kimesema kuwa kitasusia matokeo hayo kwakuwa uchaguzi haukuwa huru na haki.

Katika hatua nyingine tume ya waangalizi wa jukwa la SADC-ECF wenyewe wamepongeza jinsi zoezi la upigaji kura na uchaguzi wenyewe ulivyoendeshwa huku wakiimwagia sifa tume ya uchaguzi kwa kufanikisha zoezi hili katika kipindi kifupi.

Balozi Bethuel Kiplagat ambaye ni mwenyekiti wa tume ya waangalizi toka jumuiya ya COMESA ameonesha kuridhishwa na zoezi la uchaguzi ikilinganishwa na mwaka 2008.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.