Pata taarifa kuu
MISRI-CAIRO

Uamuzi wa Mahakama kuu Cairo kuzuia Muslim Brotherhood waigawa Misri

Wananchi wa Misri wameendelea kugawanyika kufuatia uamuzi wa mahakama kuu mjini Cairo kuamua kuzuia shughuli zozote za kisiasa za chama cha Muslim Brotherhood pamoja na kuagiza mali zake kushikiliwa.

Baadhi ya wafuasi wa Muslim Brotherhood wakiwa katika moja ya maandamano ya hivi karibuni.
Baadhi ya wafuasi wa Muslim Brotherhood wakiwa katika moja ya maandamano ya hivi karibuni. www.csmonitor.com
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo wa mahakama pia unazuia makundi yenye uhusiano na chama hicho pamoja na asasi zisizo za kiserikali kutojihusisha na masuala ya siasa nchini humo, uamuzi ambao unakigusa hata chama cha Freedmo and Justice.

Uamuzi huu unakuja mwezi mmoja baada kufanyika kwa Oparesheni ya kuwasaka wafuasi wa Muslim Brotherhood waliokuwa wamepiga kambi jijini Cairo kutaka kurudishwa madarakani kwa kiongozi wao Mohammed Morsi.

Hata hivyo, chama cha Muslim Brothehood kina uwezo wa kuwasilisha uamuzi huo katika Mahakama ya Rufaa.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa uamuzi huu wa serikali ya Misri, haukuwa sahihi hasa kipindi hiki ambacho siasa za nchi hiyo bado ni tete na kwamba jeshi linaendelea kutumia mabavu kutafuta suluhu.

Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood walikuwa katika maandamano makubwa katika kipindi cha mwezi uliopita wakipinga kuondolewa madarakani kwa raisi Mohamed Morsi hatua ambayo ilitekelezwa na majeshi ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.