Pata taarifa kuu
DRCONGO-M23

Hatimaye serikali ya Kinshasa na kundi la M23 wasaini makubaliano ya amani

Hatimaye serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imetia saini makubaliano ya amani na waasi wa kundi la M23 waliokuwa wakipigana na jeshi la serikali FARDC huko mkoani Kivu ya Kaskazini Mashariki mwa DRCongo. Makubaliano hayo yamesainiwa jana alhamisi jijini Nairobi nchini Kenya ambapo wawakilishi mbalimbali kutoka ndani na nje ya bara la Afrika walishuhudia zoezi hilo.

REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Kusainiwa kwa makubalinao hayo kunakuja baada ya Kinshasa kukubali wito wa kimataifa wa kumaliza mzozo na M23 baada ya makubaliano hayo kushindwa kusainiwa hapo awali.

Kulingana na makubaliano hayo sasa M23 itakubaliwa kuwa chama cha Kisiasa, kujumuishwa kwa wapiganaji wa M23 katika jeshi la serikali, lakini pia kuachiwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa kutoka kundi hilo.

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa katika ukanda wa maziwa makuu Bi. Mary Robinson ameelezea kuridhishwa kwake na makubaliano hayo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ukanda wa maziwa makuu ambaye ni rais wa Uganda, Yuweri Museveni, na raisi wa Malawi Joyce Banda, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, walisaini mkataba huo kama wadhamini.

Andiko lililosainiwa limetoa wito kwa Washirika wa Kimataifa hususani Umoja wa Mataifa UN na Umoja wa Afrika AU kutoa ushirikiano kwa serikali ya DRCongo ili kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa.

Wakati huo huo mashirika ya kiraia Mashariki mwa DRC yamesema kuwa hayauridhii mkataba huo kufuatia kuwa na mambo maengi ambayo itakuwa vigumu kwao kuyaelewa kwani wanahisi kama serikali ya Kinsahsa imeshinikizwa kufikia makubaliano hayo.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International, Naibu Mwenyekiti wa Mashirika hayo Omar Kavota amesema kuna baadhi ya vipengele havijawekwa wazi likiwamo suala la hatma ya viongozi wa M23 ambao wanatafutwa na mahakama wakikabiliwa na tuhuma za uhalifu..

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.