Pata taarifa kuu
TANZANIA-KATIBA

Serikali ya Tanzania yatangaza majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba linalo tarajiwa kuanza shughuli zake Februari 18 ijayo

Serikali ya Tanzania imetangaza majina ya wajumbe walioteuliwa kushiriki bunge la katiba linalotarajiwa kuanza tarehe 18 ya mwezi huu mjini Dodoma. Majina hayo yametangazwa ijumaa jioni na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Florence Turuka mbele ya waandishi wa habari ikulu jijini Dar es salaam.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa bunge ni Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Wajumbe 201 walioorodheshwa kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

Majina hayo yametangazwa siku moja toka Rais wa nchi hiyo Jakaya Mrisho kikwete kuwaonya watakaoteuliwa kusimamia maslahi ya Taifa na kuweka kando itikadi zao.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Vyama vya siasa siku ya alhamisi jijini Dar es salaam, Rais Kikwete alisema Watanzania wanatarajia kuona mchakato huo ukiendeshwa kwa amani na utulivu hivyo wajumbe wote na vyama vya siasa watangulize mbele maslahi ya Taifa badala ya kuweka mbele maslahi binafsi au ya vyama vyao.

Bunge la katiba litakutana kwa siku 70 na huenda likaongezewa siku 20 zaidi endapo hakutakuwa na maafikiano ili kujadili rasimu ya pili ya katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.