Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Kundi la Boko Haram laendelea kunyooshewa kidole cha lawama

tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu imelaumu vikali mauaji yanayotekelezwa na kundi la kigaidi la Boko Haram Nchini Nigeria na kuelezea kuwa hali hiyo haikubaliki. Hayo yanajiri huku Jeshi la Nigeria likisema kuwa litaendelea na harakati zake dhidi ya kundi hilo la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram licha ya kundi hilo kuzidisha mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia mwanzoni mwa Juma Hili katika jimbo la Borno.

Uharibifu uliyotekelezwa na kundi la Boko haram mwishoni mwa juma liliyopita, nchini Nigeria,
Uharibifu uliyotekelezwa na kundi la Boko haram mwishoni mwa juma liliyopita, nchini Nigeria, RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika jimbo la Borno, wapiganaji hao waliwaua watu 106 akiwemo nyanya mmoja aliyekuwa anajaribu kumlinda mjukuu wake kutokana na mashambulizi.

Jeshi linasema kuwa magaidi hao ambao hulenga kijiji baada kingine na kufanya mashambulizi ya kuvizia, ni wale wanaotoroka mashambulizi ya majeshi katika maficho yao mpakani mwa nchi hiyo na nchi jirani.

Jeshi lilifahamisha hivi karibuni kwamba limeshindwa kukabiliana vilivyo na mashambulizi ya wanamgambo wa Boko haram, na limeomba usaidizi wa haraka, alithibitisha mkuu wa jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, katika mazungumzo na rais Goodluck Jonathan.

Mkuu huyo wa jimbo la Borno, Kashim Shettima alijielekeza juzi katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kwa mazungumzo na rais pamoja na viongozi wa jeshi, kufuatia mauaji ya watu 106 yaliyotokea jumamosi juma liliyopita katika jimbo la Borno, shambuliyo ambalo liliwalenga jamii ya wakristo waishio katika kijiji cha Izghe.

“Tumekabiliwa na vita. Na hilo ndilo limenileta hapa ili niongeye na rais, alisema Kashim Shettima, katika mkutano na waandishi wa habari, baada ya mazungumzo na rais Goodluck.

“Nilimueleza rais wazi kwamba wanamgabo wa Boko Haramu wamejidhatiti zaidi kijeshi kuliko vyombo vya usalama”, alisema Kashim Shettima, huku akibaini kwamba endapo wanajeshi hawatapatishiwa uwezo wa kutosha na idadi ya wanajeshi wengine ikaongezwa, kamwe Boko Haramu haitoshindwa.

Jeshi nchini Nigeria lilisema juzi katika tangazo liliyotoa kwamba limeongeza idadi ya wanajeshi wa angani na aridhini katika “misitu na vijiji” ambako wanajificha wanamgambo wa Boko Haram

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.