Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINE-AMNESTY INTERNATIONAL

Amnesty International yaituhumu Israeli kutekeleza mauaji ya raia wa Palestina

Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty International limeituhumu israeli kwamba imehusika kwa ukiukwaji mkubwa kwa kuauwa maelfu ya raia wapelestina katika ukingo wa Cisjordania katika kipindi cha miaka mitatu. Jeshi la Israeli limejibu, katika tangazo liliyotoa, ambamo limelinyooshea kidole shirika hilo na kudai kwamba Amnesty International linasahau kwa makusudi matukio ya vitendo viovu na machafuko vinavyotekelezwa na raia wa Palestina dhidi ya waisraeli

Wanajeshi wa Israeli katika ukingo wa Cisjordania.
Wanajeshi wa Israeli katika ukingo wa Cisjordania. RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Israel inadaiwa kuwaua maelfu ya raia kwenye eneo la ukanda wa Magharibi katika kipindi cha miaka 3 iliyopita na kuonesha kutokuguswa na kuheshimu haki za binadamu, ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu duniani Human Rights Watch imesema.

Ripoti hiyo ya Amnesty International imeeleza namna ambavyo wanajeshi wa Israel wamekuwa wakitumia nguvu kuwakabili waandamanaji wa Kipalestina kwenye eneo la ukanda wa magharibi na kuua watu 45 ambao hata hawakuwa wamevuka mpaka.

Tayari Serikali ya Israel imejibu ripoti hiyo na kusisitiza kuwa shirika Amnesty International halikufanya uchunguzi kuonesha namna ambavyo mashambulizi dhidi ya wanajeshi wake yalivyoongezeka na kwamba wamekuwa wakitumia risasi za moto pale maisha ya wanajeshi wake yanapokuwa hatarini.

Amnesty International imeituhumu pia Israeli kutoendesha uchunguzi wa kina na uliyo huru, ambao unaendana na taratibu za kimataifa, na vile vile kutowaadhibu wanajeshi wake, ambao walihusika katika matukiyo hayo mabaya dhidi ya raia wa Palestina.

Shirika hilo imeiomba Israeli kuendesha uchunguzi uliyo huru na wazi kwa matukio ya mauaji ya raia wa Palestina yaliyotekelezwa na jeshi lake, bila kusahau maelfu ya raia waliyojeruhiwa katika mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na jeshi la Israeli.

Katika jibu lake jana jioni, jeshi la Israeli limesema Amnesty International imeonyesha kuwa haijui matukio mabaya yaliyotekelezwa na raia wa Palestine dhidi ya wapalestina.

Jeshi limebaini kwamba katika mwaka 2013 mashambulio ya kutupa mawe yaliyoendeshwa na raia wa Palestina yaliongezeka maradufu, waisraeli 132 walijeruhiwa mwaka jana. Jeshi hilo limehesabu mashambulio 66 ya kigaidi yaliyoendeshwa dhidi ya waisraeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.