Pata taarifa kuu
RWANDA-Siasa

Rais wa Rwanda awatahadharisha kwa mara nyingine tena wapinzani wake

Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa mara nyingine tena amewaonya wapinzani wake wa kisiasa waishio uhamishoni kuachana kuisaliti Rwanda.Kiongozi wa Rwanda ametoa kauli hiyo jijini Kigali wakati akiwahotubia zaidi ya maafisa 400 wa polisi kuhusu usalama wa nchi hiyo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame RFI
Matangazo ya kibiashara

Kagame amesisitiza kuwa kinachompa wakati mgumu ni maendeleo ya Wanyarwanda na wala sio watu aliwaita maadui wa nchi hiyo waliokimbilia katika mataifa kigeni wanakopewa hifadhi ya kisiasa.

Kauli ya Kagame inakuja wakati huu kukiwa na mgogoro wa Kidiplomasia kati ya Rwanda na Afrika Kusini, baada ya mataifa yote mawili kuwafukuza wawakilishi wa mataifa yao jijini Kigali na Pretoria baada ya maakaazi ya mkuu wa zamani wa Majeshi ya Rwanda Fautsine Kayumba Nyamwasa anayepewa ghifadhi nchini Afrika Kusini kuvamiwa jijini Johannerburg.

Pretoria inasema uchunguzi wao unaonesha kuwa uvamizi wa Nyamwasa ulipangwa na baadhi ya maafisa wa ubalozi wa Rwanda na Burundi, tuhma ambzo Kigali imekanusha.

Afrika Kusini nayo imesema haitamvumilia yeyote atakayevamia nchi yake na kuwashamabulia wakimbizi wa kisiasa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.