Pata taarifa kuu
CHINA-MALAYSIA-Maandamano

Raia wa China waandamana mbele ya ubalozi wa Malaysia

Raia 200 wa China wameandamana jana wakiwa na hasira na huzuni mbele ya ubalozi wa Malaysia mjini Pekin, baada ya kutangazwa kwamba ndege ya Malaysia Airlines ambamo walikuwemo ndugu zao, ilifanya ilianguka ndani ya bahari Hindi.

Waandamanaji mbele ya ubalozi wa Malaysia mjini Pekin.
Waandamanaji mbele ya ubalozi wa Malaysia mjini Pekin. AFP/Goh CHAI HIN
Matangazo ya kibiashara

“Turejesheye ndugu zetu”, hayo ni maneno yaliyokua yakitamkwa na waandamanaji mbele ya ubalozi wa Malaysia, huku kukionekana idadi kubwa ya askari polisi.

Baadhi ya waandamanaji wamejaribu kupenya ili waingiye ndani ya jengo la ubalozi wa Malaysia, bila mafanikio.

Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak ametangaza rasmi kuwa ndege ya taifa hilo aina ya MH370 iliyopotea hivi karibuni, ilianguka kwenye bahari ya hindi kusini mwa bara la Australia ikiwa na abiria 239.

Akiwa mwenye huzuni, waziri mkuu Razak amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa moya walizozipata kupitia njia ya Sattelite wamepata uhakika kuwa ndege hiyo iliishiwa mafuta ikiwa kwenye eneo la bahari ya hindi na kuanguka.

Waziri mku Razaki amewataka wanafamilia waliopoteza ndugu zao kuwa na subira wakati huu wakisubiri uhakika zaidi toka kwa vikosi vya wanamaji wa Australia ambao walifanikiwa kubaini eneo ambalo ndege hiyo inadaiwa kuanguka.

Magazeti ya nchi hiyo hii leo kwenye kurasa zao yamechapicha majina ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo huku yakisubiri kupata taarifa rasmi za uthibitisho toka kwa mamla zinazoendelea na uchunguzi kwenye bahari ya hindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.