Pata taarifa kuu
MALAYSIA

Utafutaji wa ndege ya Malaysia waendelea bahari Hindi

Watafutaji wa ndege ya Malaysia iliyopotea, wameendelea na utafiti wa kina kwenye eneo jipya la bahari ya Hindi leo Jumamosi wakitumaini kuokoa baadhi ya mabaki ya ndege hiyo MH370 baada ya picha kadhaa kuibua matumaini. 

picha ya satelite ikionesha vitu vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege hiyo
picha ya satelite ikionesha vitu vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege hiyo rfi
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo licha ya kuwa vifaa vinavyotakiwa, Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott amesema timu hiyo inakabiliwa na kazi ya kutisha kutokana na umbali wa eneo husika.

Ndege za mataifa mbalimbali zinazoshiriki operesheni ya kuitafuta ndege hiyo zilibaini vitu mbalimbali vikielea juu ya maji jana Ijumaa, baada ya mwelekeo wa utafutaji kuelekezwa katika ukanda mpya .

Kwa sasa takwimu mpya zinazoonesha kwamba ndege hiyo ilisafiri kwa mwendo kasi kuliko ilivyodhaniwa hapo awali kabla ya kupotea tarehe 8 mwezi Machi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.