Pata taarifa kuu
URUSI-CRIMEA-Diplomasia

Urusi imepunguza idadi ya wanajeshi wake katika kisiwa cha Crimea

Urusi imeondoa baadhi ya wanajeshi wake karibu na jimbo la Crimea katika mpaka na Ukraine. Wizara ya Ulinzi inasema wanajeshi hao wamerudi katika kambi yao baada ya kumaliza mazoezi lakini haikufahamika ikiwa wanajeshi wote katika mpaka huo wataoendolewa.

Jeshi la Urusi katika kambi ya zamani ya wanajeshi wa Ukraine ya Perevalnoyia.
Jeshi la Urusi katika kambi ya zamani ya wanajeshi wa Ukraine ya Perevalnoyia. Patrick Sauce - BFMTV
Matangazo ya kibiashara

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema rais wa wa Urusi Vladimir Putin alimwambia kuwa ameagiza kuyaondoa baadhi ya majeshi yake katika jimbo la Crimea.

Haya yanakuja siku moja baada ya Marekani na Urusi kushidnwa kupata mwafaka kuhusu mzozo wa Ukraine katika kikao cha mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa hayo mawili kilichofanyika jijini Paris.

Baada ya matokeo ya kura ya maoni 17 machi, ambapo raia wa Crimea walipiga kura ya kujiunga na Urusi kwa asilimia 96.

Bunge la Crimea, muda mchache baadae lilitangaza kwamba Crimea imejitenga na Ukraine na kuomba rasmi kujiunga na Urusi.

Hali hio ilipelekea mataifa saba tajiri duniani kuichukulia vikwazo Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.