Pata taarifa kuu
MALAYSIA-utafutaji ndege

Utafutaji wa ndege ya Malaysia waelekezwa eneo la viashiria vilivyobainiwa na meli ya China

Australia imesema ina matumaini kuhusu viashiria viliyogunduliwa na meli ya China ambayo inaitafuta ndege ya Malaysia MH370, lakini imetahadharisha kuwa bado hakuna ushahidi kwamba viashiria hivyo vimepatikana kutoka kwenye sanduku nyeusi ya ndege iliyopotea. 

Meli ya china ikisaidia katika shughuli za kutafuta mabaki ya ndege ya Malaysia
Meli ya china ikisaidia katika shughuli za kutafuta mabaki ya ndege ya Malaysia www.scmp.com
Matangazo ya kibiashara

Viashiria hivyo vina wiana na kipimo kilichotumiwa na taa za dharura zilizopachikwa kwenye kinasa taarifa cha ndege hiyo boeing 777, watengenezaji wa ndege hiyo wamesema.

Utafutaji wa ndege hiyo, ambayo ilitoweka wakati ikisafiri kati ya Kuala Lumpur na Beijing Machi 8, umeongezeka wakati muda ukizidi kusonga ili kupata sanduku jeusi, pamoja na betri ambayo huwasha taa za kuashiria hali ya hatari ambazo huisha nguvu baada ya siku 30.

Ndege na meli zimeelekezwa kwenye eneo ambapo meli ya China iliona viashiria sambamba na sanduku jeusi la taa za dharura wakati wa utafutaji wa meli hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.