Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Rasimu ya katiba mpya nchini Zimbabwe kuweka ukomo wa miaka kumi kwa uongozi wa rais.

Wabunge nchini Zimbabwe wamekamilisha rasimu ya katiba ambayo inapunguza madaraka ya rais na kuweka ukomo wa uongozi kwa miaka kumi, hatua hii ikiwa ni sehemu ya mageuzi muhimu kabla ya uchaguzi, mmoja wa mawaziri nchini humo amebainisha.

Wabunge wa bunge la Zimbabwe wakiwa katika kikao huko Harare
Wabunge wa bunge la Zimbabwe wakiwa katika kikao huko Harare rawstory.com
Matangazo ya kibiashara

Rasimu hiyo ambayo itapigiwa kura ya maoni, ameandaliwa na wataalamu kutoka vyama vikuu vya kisiasa katika serikali ya mseto ambayo imekuwa madarakani tangu kutokea kwa ghasia za uchaguzi mwaka 2008.

Rais Robert Mugabe,mmoja wa viongozi wa Afrika aliyeongoza kwa muda mrefu ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 32 alilazimishwa kuingia katika mpango wa kugawana madaraka na mpinzani wake Morgan Tsvangirai ili kuepusha umwagaji damu nchini humo.

Miezi ya hivi karibuni rais Mugabe amekuwa akijaribu kujiondoa katika mpango wa kugawana madaraka, akitaka kufanyika kwa uchaguzi pasipo kuwa na katiba mpya.

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.