Pata taarifa kuu
EU-ZIMBABWE

Umoja wa Ulaya EU yawaondolewa vikwazo baadhi ya marafiki wa rais Mugabe

Umoja wa Ulaya EU, umetangaza kuwaondolea vikwazo baadhi ya marafiki wa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe huku ikiendelea kumuwekea vikwazo rais Mugabe mwenyewe na wenzake wengine kumi.

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Reuters/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Ulaya imesema kuwa imefikai uamuzi huo baada ya kujiridhisha na zoezi la upigaji kura kwenye rasimu mpya ya katiba ambapo waliokuwa marafiki wa rais Mugabe walionesha ushirikiano kwenye zoezi hilo.

Licha ya kutangaza kuwaondolea vikwazo watu hao, Umoja huo imewaorodhesha watu wengine kumi akiwemo rais Mugabe mwenye ambao hawatahusika na msamaha huo.

Kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo havitamuhusu rais Mugabe na watu wake wa karibu na hivyo ataendelea kuwemo kwenye orodha ya watu ambao Umoja wa Ulaya bado inawachukulia kama watu wanaokwamisha mabadiliko ya kidemokrasia nchini Zimbabwe.

Wakati Umoja wa ukiwaondolewa vikwazo baadhi ya marafiki wa Mugabe, nchi ya Marekani yenyewe imesema bado inafikiria uamuzi wa kuiondolea vikwazo nchi hiyo licha ya kueleza kufurahishwa na mabadiliko ambayo yameanza kujitokeza nchini humo.

Vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia dhidi ya Zimbabwe vilitangazwa rasmi mwaka 2002 na nchi za magharibi kufuatia machafuko yaliyoshuhudiwa mara baada ya uchaguzi mkuu ulileta Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.