Pata taarifa kuu
Jua Haki Zako

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yakumbwa na uhaba wa fedha

Imechapishwa:

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa mashirika ya misaada yanakabiliwa na uhaba wa fedha, na kwamba yanahitaji dola milioni 400 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Muonekano kutoka angani wa kambi ya watu waliohamishwa makazi si mbali na Goma, nchini DRC.
Muonekano kutoka angani wa kambi ya watu waliohamishwa makazi si mbali na Goma, nchini DRC. © AFP/Guerchom Ndebo
Matangazo ya kibiashara

Katika kongamano la siku tatu kuhusu wakimbizi huko Geneva, Wiki iliyopita, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi, alisema asilimia 75 ya wakimbizi wanaishi katika nchi maskini na zile zinazoendelea.

Grandi ameiomba jamii ya kimataifa kutofumbia macho mamilioni ya waliokimbia makazi yao huko Ukraine, Sudan, Syria, Afghanistan, na vile vile DRC.

Kuzungumzia haya na pia haki za wakimbizi kwa ujumla, Bi. Faith Kasina, msimamizi wa UNHCR ukanda wa Afrika mashariki alizungumza na George Ajowi.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.