Mjadala wa Wiki
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
DRC yampata Waziri Mkuu baada ya kusubiri miezi mitano
Hatimaye rais wa DRC Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga kuwa Waziri Mkuu. Hii inakuja baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya rais huyo na mwenzake wa zamani Joseph Kabila. Matarajio ya raia wa DRC ni nini ?23/05/201912:12 -
Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu ataka maandamano dhidi ya rais Tshisekedi
Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu, anataka maandamano yafanyike nchini humo kumshinikiza rais Felix Thisekedi aondoke madarakani kama ilivyokuwa nchini Sudan na Algeria.Fayulu anasema yeye ndiye aliyeshinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018.Tunachambua hili kwa kina.02/05/201915:18 -
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu
Baada ya kuwa madarakani kwa miaka 20 hatimaye Abdulaziz Bouteflika amelazimika kusalimu amri na kujiuzulu kama rais wa nchi wa Algeria.Nini hatima ya nchi ya Algeria baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 ambaye tangu mwaka 2013 amekuwa akitumia gari la magurumu baada ya kupatwa na kiharusi.Kwa mujibu wa Katiba, Spika wa Senate sasa ndio rais wa muda hadi pale Uchaguzi mpya utakapofanyika.03/04/201912:01 -
IS ladhoofishwa Syria na Iraq
Baada ya miezi ya mapigano, kikundi cha jihadi cha Kiislam (IS) kimepoteza Baghuz, kijiji cha mashariki mwa Siria ambacho kinaelezwa kuhitimisha utawala wa kihalifa nchini syria.Kama ambavyo mwishoni mwa 2017, IS ilivyopoteza ngome zake za Mosul nchini Iraq na Raqqa nchini Syria.27/03/201912:55 -
Mvutano kati ya Rwanda na Uganda Marekani yatia neno
Makala ya mjadala inaangazia mvutano wa kidiplomasi akati yamataifa mawili ya Afrika mashariki,Uganda na Rwanda wakati huu jumuiya ya Afrika mashariki ikiwa kimya..wachambuzi Abbas Mwalimu na Haji Kaburu wanadadavua kwa kina.13/03/201912:12 -
Mzozo kati ya Rwanda na Uganda kuhusu mpaka wa Katuna
Nchi za Rwanda na Uganda zinashuhudia mvutano wa kidiplomasia. Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuwaficha maadui wa serikali yake, suala ambalo Uganda inakanusha vikali.06/03/201911:29 -
Mustakabali wa DRC baada ya matokeo ya uchaguzi
Baada ya tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kumtangaza mshindi wa kiti cha uraisi mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi,tunaangazia nini matarajio ya raia sasa,nini mustakabali wa DRC wakati huu upinzani wa lamuka ukipinga matokeo hayo kwa kudai udanganyifu ulifanyika.31/01/201911:46 -
Mzozo wa kisiasa nchini Venezuela
Venezuela imejikuta katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi, kiongozi wa upinzani Juan Guaido amejiapisha kuwa rais, huku kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro akitishia kumchukulia hatua kali. Tunajadili hili kwa kina.30/01/201911:35 -
Wananchi wa DRC bado wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu
Mamilioni ya raia wa DRC, pamoja na dunia, inasubiri Tume ya Uchaguzi kumtangaza mshindi wa Uchaguzi wa urais, baada ya wananchi kupiga kura Desemba 30 2018. Nani atashinda Uchaguzi huu na ni kwanini matokeo yamechelewa ? Tunachambua suala hili kwa kina.09/01/201917:01 -
Raia wa DRC waendelea kusubiri matokeo,mtandao wazimwa
Makala ya mjadala wa wiki inaangazia hali ya mambo nchini DRC wakati huu raia wakisubiri matokeo ya kura ya uraisi wabunge na viongozi wa wilaya kote nchini humo kunashuhudiwa mtandao ukizimwa kwa sababu kiusalama kama ambavyo serikali imeeleza...karibu,wazungumzaji ni Cyllile Muhongya na Jaribu muliwavyo wote wakiwa Mashariki mwa DRC.02/01/201911:43 -
DRC ipo tayari kwa Uchaguzi wa Desemba 30, 2018 ?
Wananchi wa DRC, wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais mpya na viongozi wengine, baada ya zoezi hilo kuahirishwa kwa wiki moja baada ya kuteketea kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili, tukiwa na Steven Chondo, mmoja wa maafisa wa kampeni wa mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary, lakini pia Reubens Mikindo , Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani UDPS, ambacho mgombea wake ni Felix Tshisekedi.26/12/201817:07 -
Wananchi wa DRC kupiga kura siku ya Jumapili
Wananchi wa DRC watapiga kura siku ya Jumapili, kumchagua rais mpya. Kampeni zinamalizika wiki hii kuelekea Uchaguzi huo wa kihistoria.19/12/201814:01 -
Marekani: Democratics washinda bunge la wawakilishi, Republican watawala Senate
Chama cha Republican cha rais Donald Trump, kimepata ushindi katika bunge la Senate huku kile cha Denocratic, kikirejesha udhibiti wa bunge la wawakilishi, baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Wabunge, Maseneta na Magavana, uliofanyika siku ya Jumanne. Matokeo haya yanamaanisha nini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kujadili hili, ni Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa mjini Arusha nchini Tanzania na Dokta Brian Wanyama, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kibabii mjini Bungoma nchini Kenya.07/11/201813:13 -
Rais Paul Biya achaguliwa tena kuongoza Cameroon kwa muhula wa saba
Rais wa Cameroon Paul Biya, ametangazwa mshindi kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa saba, kuendeleza uongozi wake wa miaka 36. Upinzani umekataa kutambua ushindi huu. Ushindi huu una maana gani kwa demokrasia ya Cameroon na bara la Afrika ? Tunajadili.24/10/201813:03 -
Siasa za mashine za kupigia kura nchini DRC
Kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, bado kuna mvutano wa matumizi ya mashine za kupigia kura. Wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia yanataka zisitumiwe kwa hofu ya wizi wa kura, lakini Tume ya Uchaguzi CENI, inasisitiza kuwa ni sharti zitumiwe. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ili mwafaka kupatikana. Tunajadili hili kwa kina.10/10/201814:14
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.