Talisman Brisé
Talisman Brisé ni tamthilia ya redio inayosimulia hadithi ya mtunza bustani Kwame ambaye bosi wake Profesa Omar anatekwa nyara na watu wasiojulikana. Kwa nini Profesa Omar anatekwa nyara na watu hao? Mfanyakazi wake Kwame atafanikiwa kumuokoa Bosi wake? Fuatilia haya kwenye tamthilia ya Talisman Brise hapa rfi kila siku ya jumapili ndani ya Makala ya Changu Chako Chako Changu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
- 1
- 2
Vipindi vyote
-
Kwame ajibu maswali ya polisi
Kule kituoni, polisi wawili wanamuuliza masuali mazito. Ana jaribu kujibu kama anavyowezo. Mwishoni wanamwachia. Wakati anapoondoka anapata habari kuwa wateka nyara wa profesa Omar wanaomba pesa ili wamwachie huru (Sehemu za harakati - maswali)26/02/201202:42 -
Kwame hana uaminifu na mtu
Kwamé hamuamini mtu na anaamua kupeleleza mwenyewe. Lakini anakamatwa na polisi ambao wanampeleka kituoni. Haelewi vizuri wanamtakia nini na anaishia mahabusu. Nathalie anamkana...(Sehemu za harakati - kufungwa)19/02/201202:42 -
Kwame anakutana na polisi wa kike,je atamsaidia kumpata Profesa Omar?
Katika muendelezo wa mchezo huu Kwame bado anaendelea na jitihada za kubaini wapi alipo Profesa Omar,ambapo leo anakutana na askari kujua nini kitajiri fuatilia mchezo huu.12/02/201205:24 -
Nini kitampata Kwame baada ya kufika Tondiedo?
Kwame bado anaendelea na jitihada zake za kumtafuta Proffesa Omar huko Tondiedo, Je atafanikiwa kumpata? fuatilia makala haya .05/02/201205:24 -
Kwamé anakutana na Clément
Kule Tondiedo, Kwamé anakutana na Clément, mtembezaji wa watalii na mwanafunzi Chuo Kikuu cha Niamey. Anamjua Profesa Omar. Hii inaweza kuwa sehemu ya kuanzia...Jioni kwenye mgahawa, anasikia sauti ambayo si ya kawaida inayomfuata...halafu kule redioni wanazungumzia kutekwa nyara kwa Professa na GIETA, shirika lisilo la serekali linalo dhamini tafiti za profesa. Kwamé, hawaamini.29/01/201205:24 -
Episode ya pili
Baada ya kutekwa nyara kwa Profesa Omar, Kwamé anaamua kwenda Tondiedo kwa ajili ya kupata faharasa. Lakini pikipiki inaharibika, halafu, mtu wa ajabu ambaye anadhani anamfahamu anamzuia...22/01/201205:24 -
Kwame mtunza bustani yuko katika bustani mara wageni wanaingia.
Kwamé, mtunza bustani kwenye kituo cha utafiti wa kilimo, Gorom Gorom, anahadithia hadithi yake kwa shangazi yake: Huku akiwa anafanya kazi kwenye bustani, bosi wake, Profesa Omar anatekwa nyara huku yeye akishuhudia...(Sehemu za harakati - uhoga).15/01/201205:24
- 1
- 2
Talisman Brisé
Talisman Brisé ni tamthilia ya redio inayosimulia hadithi ya mtunza bustani Kwame ambaye bosi wake Profesa Omar anatekwa nyara na watu wasiojulikana. Kwa nini Profesa Omar anatekwa nyara na watu hao? Mfanyakazi wake Kwame atafanikiwa kumuokoa Bosi wake? Fuatilia haya kwenye tamthilia ya Talisman Brise hapa rfi kila siku ya jumapili ndani ya Makala ya Changu Chako Chako Changu.