Pata taarifa kuu
BAHRAIN

Polisi wakabiliana na waandamanaji nchini Bahrain

Vikosi vya nchini Bahrain vimewamwagia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira waandamanaji waliokussanyika kwa ajili ya kuadhimisha mwaka mmoja wa maandamano ya kudai Demokrasia.

Baadhi waandamanaji nchini Bahrain wakiandamana kudai demokrasia
Baadhi waandamanaji nchini Bahrain wakiandamana kudai demokrasia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya askari na wanakikosi wengine wa usalama wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini humo, huku waandamanaji hao wakionesha nia ya kuendelea kusonga mbele bila kujali kikwazo cha wwanausalama.

Waandamanaji wengi wao kutoka madhehebu ya kishia wanashinikiza kuwepo utawala wa kikatiba nchini humo,maandamano ambayo yamesababisha wau 60 kupoteza maisha tangu kuanza kwa maandamano hayo mwezi Februari mwaka jana.

Nayo serikali ya Mfalme wa nchi hiyo Hamd bin Isa al Khalifa imesema kuwa inatekeleza majukumu yake ya kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini Bahrain.

Maandamano hayo ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa maandamano ya kudai demokrasia yaliitishwa na wanaharakati wa upinzani yakiwa na lengo la kushinikiza upatikanaji wa demokrasia nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.