Pata taarifa kuu
Bahrain

Shirika la Amnesty International lakemea hukumu iliyotolewa na Bahrain dhidi ya Wanaharakati nchini humo

Polisi nchini Bahrain wamepambana na waandamanaji wa kishia waliokuwa wakipinga hukumu ya kifungo dhidi ya Wapinzani maarufu, Mashuhuda na Wapinzani nchini humo wameeleza.

Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalfan
Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalfan
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya polisi vilitumia Gesi ya kutoa machozi na Risasi za mpira kuwatawanya Waandamanaji waliokuwa wameficha nyuso zao wakichoma Magurudumu na mapipa ya takataka katika Maeneo ya kuelekea katika Vijiji vya Washia, Magharibi mwa Mji wa Manama.

Mtu moja alijeruhiwa vibaya wakati wa purukushani hizo mjini Karrana baada ya kupigwa Risasi, Wapinzani wa kishia wameeleza.

Wizara ya Mambo ya ndani ya Bahrain alieleza kwenye mtandao wa kijamii wa Tweeter kuwa mtu huyo aliyejeruhiwa yu hospitalini na kuwa Mamlaka inafanyia Uchunguzi shambulio hilo.

Waandamanaji wanadai kuwa hukumu dhidi ya wapinzani hao si ya haki, wakitoa wito kwa Mahakama ya Rufaa kutengua adhabu hiyo dhidi ya Wanaharakati 13, wakiwemo saba wanaokabiliwa na kifungo cha Maisha.

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadam Amnesty International hapo jana lilishutumu hukumu hizo na kusema kuwa Serikali haiko kwenye njia sahihi ya kufanya mabadiliko isipokuwa imekuwa ikiendeshwa kwa Visasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.