Pata taarifa kuu
IRAQ

Jeshi la Iraq lakabiliana na wapiganaji wa Kisunni mjini Tikrit

Jeshi la Iraq limekabiliana na wapiganaji wa Kislamu wa ISIL karibu na mji wa Tikrit katika juhudi za kujaribu kuwatokomeza wapiganaji hao wa Kisunni wanaodhibiti miji kadhaa Kaskazini na Magharibi mwa nchini hiyo.

Wanajeshi wa Iraq wakiwa chonjo wakati wa makabiliano yao
Wanajeshi wa Iraq wakiwa chonjo wakati wa makabiliano yao REUTERS/Mushtaq Muhammed
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo yalishuhudiwa baada ya Waziri Mkuu Nuri al-Maliki kukiri kuwa maamuzi ya kisiasa yatachukuliwa kuwashinda wapiganaji hao ambao kwa kipindi cha mwezi mmoja wamewaua zaidi ya watu 1,000 katika mikoa mitano nchini humo.

Jeshi la Iraq linasema liliwasili katika mji huo siku ya Alhamisi likiwa limejihami kwa ndege za kivita na mapigano hayo yameendelea hadi siku ya Ijumaa.

Wakati makabiliano hayo yakiendelea ,uongozi wa eneo la Kikurdi linalojitegemea umesema hautarudi nyuma katika jitihada za ujiongoza na kutoshirikiana na serikali ya al-Maliki.

Gari la kijeshi la Iraq
Gari la kijeshi la Iraq REUTERS/Ahmed Saad

Kiongozi wa Kikurdi Massud Barzani amesema, “Uongozi wa Baghdad hauwezi kuingilia maeneo yetu kwa sababu ni kinyume cha katiba ya eneo letu ambalo linajiongoza,”.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo katika kikao chake na Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza William Hague ambaye alitembelea eneo hilo katika jitihada za kuona namna ya kutatua mzozo wa Iraq.

“Tumekuwa wavumilivu kwa miaka 10 na serikali hii ya Shirikisho ili kutatua matatizo ya mipaka ya maeneo haya bila mafanikio.,” aliongezea.

Wapiganaji wa Kikurdi nchini Iraq
Wapiganaji wa Kikurdi nchini Iraq REUTERS/Yahya Ahmad

Waziri Mkuu Maliki katika mahojiano na BBC amesema ndege za kivita za Syria zimetekeleza mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa Kissuni katika mji wa Al-Qaim katika mpaka wa nchi hizo mbili.

Maliki amesema Baghdad haijaomba msaada wowote wa kijeshi kutoka nchini Syria lakini akasisitiza kuwa “anakaribisha” usaidizi kutoka kwa jirani zake katika juhudi kukabiliana na kundi la ISIL.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani na kiongozi wa Kikurdi Massoud Barzani
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani na kiongozi wa Kikurdi Massoud Barzani REUTERS/Stringer

Iraq ilikuwa imeomba ndege zisozokuwa na rubani kutoka nchini Marekani kukabiliana na wapiganaji hao lakini Marekani ikawatuma wanajeshi 300 kutoa ushauri kwa jeshi lake.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amewasili nchini Saudi Arabia kukutana na viongozi wa nchi hiyo kuzungumzia hali ya mambo nchi Iraq na Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.